31 October, 2015

Wewe ni mtumiaji wa vilevi? haya ni mambo ya muhimu unayopaswa kufahamu kuhusiana na Vilevi


“Haiuzwi kwa wenye umri chini ya miaka 18, kunywa kistaarabu” ujumbe huu unapatikana katika matangazo yote ya vilevi, na nadhani hilo linatambulika kwamba pombe si ya vijana chini ya miaka 18. Unywaji wa pombe ni kawaida kwa watu wengi lakini unakunywa kistaarabu? Sina mpango wa kukufundisha kunywa pombe wala kukushawishi uanze kunywa Pombe wote tunajua madhara yanayoletwa kwa unywaji wa pombe wa kupindukia. Leo tuongelee upande wa pili wa shilingi, faida za unywaji wa pombe kwa wastani. Narudi unywaji wa pombe kwa wastani.
Magonjwa ya Moyo.
Utafiti kutoka  Harvard University  Marekani, umegundua unywaji wa pombe kwa kiasi cha wastani kinasaidia mzunguko mzuri wa damu,hii inasaidia kuzia matatizo ya moyo na magonjwa ya kiharusi na kupooza (stroke)
Urefusha Maisha
Utafiti uliofanywa na Catholic University  huko Campobasso, waligundua kuwa kunywa chupa chini ya 4 au 2 kwa siku kwa mwanamme au mwanamke,  kwa asilimia  18 inaongeza muda wa kuishi kama  ililipotiwa na Reuters. Dr. Giovanni de Gaetano  wa Catholic University  pia alisema sio mbaya kama unaweza kunywa pombe kidogo wakati wa kula. Makala nyingine iliyoandikwa na Mediterranean diet, kuwa mvinyo (wine) ni kinywaji safii wakati wa chakula cha mchana na cha jioni. Lakini usinywe tu pombe wakati wote.
Inasaidia kuamsha Hisia za Mapenzi
Kama ilivyo Red Wine inasaidia kupunguza kasi ya magonjwa ya moyo, Mwaka 2009 jarida lililotambulika kama Sexual Medicine, liliandika kwa utafiti waliofanya  asilimia 25 – 30 wanywaji wa pombe hawapati matatizo ya kushindwa kushiriki tendo. Mkuu wa utafiti , Kew-Kim Chew Mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko kutoka University of West Australia alifanya utafiti kwa wanaume  1,770 wa Australia,  Chew aliwashauri pia wanaume hao wasitumie pombe kupitiliza sababu bado wanafanya utafiti juu ya swala hilo kwa kina zaidi.

Pombe huamsha Akili
Utafiti uliohusisha watu zaidi ya 365,000 toka mwaka 1997 iliripotiwa na jarida la Neuropsychiatric Disease and Treatment watu wanaokunywa kwa wastani wanauwezo wa kuzuia ugonjwa wa Alzheimer na magonjwa mengine ya akili. Kiwango kidogo cha pombe kinafanya seli za ubongo ziwe hai (fit/active) alisema Edward J. Neafsey, Ph.D mwandishi wa Science Daily. alisema pia hawashauri watu wasiokunywa pombe waanza kunywa pombe. Na akasema kama wale wanaokunywa wanakunywa kwa wastani basi itawasaidia.
Husaidia Tatizo La Mawe kwenye Kibofu
Kwa wanywaji wa wastani kuna uwezekano wa kupunguza uwezekano wa kupata  tatizo la mawe kwenye kibofu huo ni  utafiti uliofanywa na University of East Anglia, watafiti walisema faida zinaonekana kwa wale wanywaji wa kawaida na sio waywaji wa pombe kupinduki  sababu unywaji wa pombe kupitiliza huleta matatizo ya kiafya
Ugonjwa wa Sukari
Tafiti zilizofanywa uholanzi,  watu wenye afya wanao kunywa glass moja au mbili kwa siku wanapunguza uwezekano wa kupata aina ya pili ya kisukari ukiachilia mbali wale wasiokunywa hata kidogo, wale wanaokunywa kidogo wana afya zaidi, walisema watafiti hao kupitia Reuters.
Angalizo kujua faida hizi za pombe haina maana kama hujaanza kunywa pombe uanze sasa na kama wewe unatumia kilevi basi kunywa kwa kiwango kidogo sababu ni faida kwa afya yako kuliko unywaji wa kupindukia. Kunywa kistaarabu.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...