Upasuaji umepangwa kufanyika kwa mara ya kwanza kupandikiza uume nchini
Marekani, kwa lengo la kuwasaidia mpiganaji wa zamani. Upasuaji huo wa
saa 12- utahusisha ushonaji wa neva muhimu na mishipa ya damu kwa ajili
ya kutunza mkojo na kumuwezesha mgonjwa kufanya tendo la ngono.
Upasuaji huu unafuatia mafanikio ya kwanza kabisa ya upandikizaji wa
uume nchini Afrika kusini mwaka jana. Jopo la madaktari kutoka Hospitali
ya chuo kikuu cha Hopkins (JHU) wanapanga kumfanyia upasuaji huyo
mwanajeshi wa zamani mwenye umri wa miaka 60kama sehemu ya majaribio.
Hatua ya kwanza ya upasuaji huo itaanza kwa kuondoa uume kutoka kwa
kijana aliefariki ambaye alijitolea kutoa uume wake kwa ruhusa ya
familia yake. Kwa mujibu wa jopo la madakatari katika JHU matumaini ya
mwanajeshi huyo wa zamani ni kwamba hisia za uume wake zitarejea katika
muda wa miezi 12.
Uwezekano wa mgonjwa kupata watoto, utategemea kiwango cha jeraha na
mafanikio ya upasuaji huo. Lakini Wanasayansi wanasema kutokana na
kwamba ni upasuaji mmoja wa kupandikiza uume uliofanyika, madaktari
watakua makini kuhakikisha kuna matumaini ya kweli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment