Mapacha watano wa kike wamezaliwa Marekani katika hospitali moja ya wanawake mjini Texas Houston.Wauguzi katika hospitali hiyo wanasema kuwa uzazi huo kutokana na mimba moja ni rekodi mpya ambayo haijawahi kutokea Marekani.
Danielle Busby ambaye ndiye mama wa watoto hao ambao wamepewa majina ya
Olivia Marie, Ava Lane, Hazel Grace, Parker Kate na Riley Paige;anasema
kupata watoto hao wote wakiwa wazima kwake ni baraka ya hali ya juu.
Inasemekana watoto wengi sawa na hao walihahi kuzaliwa mara moja huko
London Uingereza ,mwaka 1969 katika hospitali ya Queen Charlotte.
Zaidi ya Madaktari na wauguzi 12 walilazimika kufanya kazi ya ziada
ilikumsaidia bi Busby kujifungua watoto hao ambao hawakuwa wametimiza
umri wa miezi tisa tumboni kwa njia ya upasuaji .
Baba wa mtoto huyo, Adam Busby amewamiminia sifa kedede wahudumu wote wa hospitali hiyo waliofanikisha operesheni hiyo.
Bwana Busby amesema kuwa mwanawao wa kwanza Blayke anawasubiri kwa hamu na ghamu.
Bi. Busby alikuwa na tatizo la kupata ujauzito hivyo akatumia mbegu pandikizi ya uzazi kwa mimba zake zote mbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment