Unyanyasaji wa watoto umeendelea kuwa
sehemu ya matukio ambayo yamekuwa yakikithiri sana ndani ya familia na
jamii za watu wengi duniani.Kitendo cha msichana wa kazi kule Uganda
kumtesa mtoto wa bosi wake kwa kumpiga bado hakijasahaulika na
mamilioni ya watu duniani baada ya kunaswa na kamera na kusambazwa
kwenye mitandano ya kijamii.
Tukio la aina kama hiyo limetokea tena kule Bulgaria baada ya muuguzi Emiliya Kovacheva kumtesa kwa kumpiga mtoto mchanga wa siku nne bila kuwa na huruma kwa madai anapiga kelele.
Mtoto huyo Nicole aliyekuwa ameachwa na mama yake alipata majeraha makubwa kufuatia mateso kutoka kwa muuguzi huyo.
Awali muuguzi huyo alikataa kuwa
amefanya kosa hilo lakini baadaye alikiri baada ya kuonyeshwa video
baada ya kamera kunasa tukio zima ndani ya humba hicho cha hospitali na
kusema alifanya hivyo kutokana na kuchanganyikiwa baada ya mtoto huyo
kukataa kulala na kuwasumbua watoto wengine waliokuwa wamelala.
Kwa sasa muuguzi huyo anakabiliwa na kosa la mauaji
No comments:
Post a Comment