Mbio
za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2017 ambazo ni za 15 tangu
Kuanzishwa kwake, zimezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam katika
mkutano na wanahabari, wadhamini na Chama Cha Riadha Tanzania.
“Tumeona
matunda ya udhamini huu kwa mfano mwaka huu tumeshuhudia mshiriki wa
Kili Marathon akishiriki katika michezo ya Olimpiki kule Brazil na
kumaliza katika nafasi ya tano katika mbio za kilomita 42. Tunaweza
kuwapata akina Simbu wengi kutoka kili Marathon na ndicho hasa wadhamini
wengi wanakitafuta,” alisema Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Kushilla Thomas
Aidha
Mkurugenzi huyo alisema wadhamini wengine wa mashindano hayo ni Tigo
ambao wanadhamini 21km, Gapco kwa 10 km-viti vya magurudumu na baiskeli
ya kunyonga kwa mkono na Grand Malt-5km. Wadhamini wengine ni pamoja na
KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC
Automobile,Keys Hotel, Air Rwanda na Anglo Gold Ashanti.
Aliishukuru
pia wizara yenye dhamana ya michezo kwa kuhakikisha miaka yote kwamba
tukio hili linafanikiwa,pia amewapongeza waandaaji, Wild Frontiers,
waratibu wa kitaifa-Executive Solutions, Chama cha Riadha Tanzania (RT),
Kilimanjaro Marathon Club, Mkoa wa Kilimanjaro na Chuo Kikuu cha
Ushirika Moshi (MoCU) kwa kuwa wenyeji wa mashindano hayo.
Kwa
upande wake, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli
zawadi kwa 42km Kilimanjaro Premium Lager Marathon ni pamoja na – jumla
ya Tsh milioni 20 kwa washindani wanaume na wanawake watakaoshika nafasi
10 za juu. Mshindi wa kwanza kutoka kila kundi atapata Tsh milioni 4
kila mmoja.
“Hatuwezi
kuwasahau wanariadha wote wa hapa nchini walioshiriki kwenye mashindano
haya na kuipa fahari nchi yetu na kuwa watashinda zawadi zote hizi
tunazozitoa. Tunaamini kwamba mashindano haya ya marathon pia yatafungua
milango kwa wanariadha wetu kwa ajili ya kushiriki mashindano ya
kimataifa ya marathon nje ya nchi yenye zawadi kubwa,” alisema Pamela Kikuli.
No comments:
Post a Comment