10 October, 2016

Matokeo ya Barani Afrika kufuzu kombe la dunia

Barani Afrika kumepigwa michezo minne ya kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia zitazofanyika nchini Urusi Mwaka 2018.Nigeria
Nigeria Super Eagle wakicheza ugenini wamewatambia wenyeji wao Zambia chipolopolo kwa kuiwachapa kwa mabao 2-1. 

Mabao ya Nigeria yakifungwa na Alex Iwobi na Kelechi Iheanacho, goli la Zambia likifungwa na Collins Mbesuma

Algeria wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wametoshana nguvu na Cameroon kwa kufungana bao 1-1.

Mafarao Misri wamewatambia Congo kwa kuwachapa kwa mabo 2-1 huku Tunisia nao wakishinda nyumbani kwa mabao 2 - 0 dhidi ya Guinea.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...