Kampuni ya Samsung imesitisha utengenezaji wa simu za Galaxy Note 7
baada ya hofu kuendelea kuwepo kuwa hata zile simu za mara ya pili
zilizodaiwa kurekebishwa zinaweza kulipuka.
Mtu anayefahamu uamuzi huo kwa ukaribu, amethibitisha kupitia CNN
usitishwaji wa muda wa simu hizo baada ya shirika la habari la Korea
Kusini, Yonhap kuripoti kwanza kuhusiana na taarifa hizo.
Tangazo hilo limekuja baada ya makampuni ya Marekani na Australia
kusema yataacha kufidia simu hizo kwa walionunua mwanzo kutokana na
wasiwasi kuwa simu hizo nazo ni vimeo kama za awali.
Mapema baada ya Galaxy Note 7 kuingia sokoni mwezi August, baadhi ya
watumiaji walidai kuwa simu zao zilikuwa zikishika moto. Kampuni hiyo
ililazimika kuziondoa sokoni simu zote kwa kudai zina tatizo la betri
linalopeleka zichemke na hivyo kuwaka moto.
Simu mbadala zilikuwa zimalize tatizo hilo na tayari baadhi ya
watumiaji walipewa zingine. Lakini baadhi ya wateja bado wamekuwa
wakiripoti kuwepo kwa tatizo hilo hatari kwenye simu zao mpya.
CHANZO:BONGO5
10 October, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment