14 October, 2016

Kocha wa Uingereza asema kikosi chake ni kibovu

Kocha wa muda wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema alirithi kikosi kibovu baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Slovenia katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia juzi. 
 Kocha wa Uingereza Gareth Southgate kushoto
Southgate alichukua mikoba ya Sam Allardyce mwezi uliopita kwa ajili ya kuisimamia timu hiyo katika mechi zake nne ambapo mpaka sasa ameshinda mchezo mmoja dhidi ya Malta kabla ya sare ya jana waliyopata. 

Uingereza ambao wanaongoza kundi F, walipata alama hiyo moja jana kufuatia juhudi za hali za juu zilizoonyeshwa na kipa wake Joe Hart. 

Southgate amesema wakati alipoichukua timu haikuwa sawa lakini taratibu anaona kama kikosi hicho kinaimarika.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...