Liverpool v Man Utd: Uteuzi wa refa Anthony Taylor wakosolewa

Anthony Taylor
Mkuu wa zamani wa marefa Uingereza Keith Hackett amekosoa uteuzi wa refa kutoka Manchester Anthony Taylor kuwa mwamuzi wa mechi ya Ligi ya Premia kati ya Liverpool na Manchester United.

Taylor huishi maili sita kutoka Old Trafford, na Hackett anaamini huenda hilo likasababisha madai wa kupendelea upande mmoja.

"Hakuna anayetilia sana uadilifu wake," Hackett alisema.

"Lakini je, kitu kikienda mrama? Itakuwa vigumu kwa baadhi kuvumilia."
Taylor hana uhusiano wowote na United lakini hushabikia klabu ya Ligi ya Taifa ya Kaskazini ya Altrincham.

Hackett anasema inashangaza ikizingatiwa kwamba Mark Clattenburg angepatikana siku hiyo ya Jumatatu.

Badala yake Clattenburg, ambaye ni shabiki wa Newcastle United, ataudumu kama mwamuzi wa nne mechi nyingine wikendi.
Tayari mashabiki wa Liverpool wameanza kulalamika mitandao ya kijamii kuhusu uteuzi wa Taylor.

Comments

Popular posts from this blog

Viashiria 6 ni kwa nini unatakiwa kubadili Maisha yako Leo

Furaha ya kweli inaletwa na wewe mwenyewe.