Tunasema asante kwa teknolojia kila siku
kwa sababu ya vitu vizuri ambavyo tunakutana navyo vikikufikia na
kurahisisha mambo mengi kwa sababu tu wataalam wamekaa na wamebuni kitu
kizuri !!
Unaambiwa ni suala la kukaa tayari
wakati wowote kuanzia sasa tutakuwa na simu zenye uwezo wa kufanya
scanning chakula na kutoa majibu kwamba kwenye chakula kuna nini na
nini…
Kwa sasa kuna kifaa kinaitwa SCiO
scanner ambacho ni kidogo tu hivi na kina uwezo wa kufanya scanning
kugundua vitu vingi kama kiasi cha sukari kwenye chakula, au mafuta,
chumvi, kemikali na vitu vingine… hiki kifaa kimeingizwa kwenye list ya
ugunduzi mkubwa uliofanywa kwa mwaka 2015.
Ukiwa na SCiO scanner kama ni mtu mwenye
tatizo la kisukari au presha inaweza kumsaidia pia kwa ajili ya kuweza
kudhibiti kula vyakula ambavyo havitakiwi kwa wakati akiwa kwenye hali
ya kuumwa.
Video ya kifaa chenyewe hii hapa.
No comments:
Post a Comment