Kampuni ya watengenezaji wa laptop za Lenovo kutoka China wamethibitisha kwamba mwaka 2016 wanakuja kuiandika rekodi mpyampya Duniani.
Lenovo wanakuja na aina nyingine ya Laptop kwa mwaka huu 2016, mzigo ni Lenovo Yoga 900 ambapo hii itakuwa ndio laptop nyepesi zaidi Duniani, ina upana wa nusu inch tu upana ambao wanaufananisha na ule wa simu ya iPhone…
kingine ni kwamba inaweza kukunjwa kwa namna yoyote bila kuvunjika na
wala haina mwisho, yani unaweza kuikunja mpaka sehemu ya nyumba ya kioo
na sehemu ya chini vikakutana na bado iko on bila kuzimwa !!
Uwezo wake pia inaweza kukaa na chaji
kwa zaidi ya saa 10, na matarajio yaliyopo ni kuziingiza sokoni mwezi
March 2016.. bei itagusa kama dola 1,100 ambazo ni sawa na Milioni 2.3
za Kitanzania.
Video hii hapa na muonekano wa Laptop hizo mpyampya.
No comments:
Post a Comment