Tanzania ni moja kati ya nchi zilizofanikiwa duniani kuratibu maabara
inayohamishika kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ebola na magonjwa
mengineyo ya mlipuko.
Maabara hii inaweza kusafirishwa mpaka kwenye maeneo yaliyoathirika,
ikiwa ndani ya masanduku yaliyofungwa vyema badala ya kusafirisha
sampuli kwa ajili ya vipimo kutoka eneo moja kwenda jingine na kuwa
katika hatari ya kuathiriwa na vijidudu vingine.
Tanzania na Nigeria ndizo nchi pekee kusini mwa Jangwa la Sahara zenye
maabara ya aina hii ambayo itakuwa msaada mkubwa pia kwa nchi za jirani
za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu,
NIMR Dokta Mwele Malecela, amesema maabara hii ina umuhimu kwa kuwa
itawezesha kufanyika kwa uchunguzi kwa urahisi na haraka zaidi, hata
katika maeneo yaliyo na ugumu kufikiwa.
Changamoto ambayo ilionekana wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola
Afrika Magharibi ni wahudumu kutofika kwa urahisi kwenye maabara kwa
ajili ya uchunguzi wa haraka kutokana na umbali na miundo mbinu mibovu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment