13 July, 2016

Unamfahamu Gyptian mkali wa reggae kutoka Jamaica?

Kwa majina yake kamili anajulikana kama Windel Beneto Edwards. Alizaliwa mnamo October 25, 1983 katika kijiji kimoja kinachojulikana kwa jina la King Weston huko Jamaica. Wazazi wake walijulikana kama Pauline(Mama) na Basil(baba) ambaye pia ni Rastafarian. Wazazi wake wote wawili hawakumzuia kijana wao huyu kufanya muziki licha ya Dini yao bali walimpatia kijana wao support na kuhakikisha anatimiza malengo yake.

 Akiwa na umri wa miaka 7, Gyptian alianza kuimba kwaya kanisani. Baada ya wazazi wake kukitambua kipaji cha kijana wao, waliamua kumtambulisha kijana huyo kwa Producer mmoja aliye julikana kwa jina la Mr. Wong kutoka katika studio iliyojulikana kama Portmore, St. Catherine-"Sikulitila jambo hili maanani" Gyptian alisema.

Akiwa chini ya usimamizi wa Mr.Wong na Mpiga guitar maarufu Earl “Chinna” Smith, Gyptian alifanikiwa kushinda shindano moja la kusaka vipaji huko Kingston. Alijipatia jana la GYPTIAN kutokana na tabia yake ya kufunga T-shirt yake kichwani kama walivyokua wakfunga wafalme wa Misri(Egypt) ambao kwa wakati ule walijulikana kama Pharaohs, Hivyo rafiki zake wakaondoa herufi 'E' kwenye jina EGYPT na kumpatia jina GYPTIAN ambalo analitumia mpaka leo hii.

Mnamo mwaka 2005 alifanikiwa kuachia ngoma kali mbili ambazo ni "Is There A Place" na "Serious Times". Na ilipofika mwaka 2006, alichaguliwa katika tuzo zilizojulikana kama "International Reggae and World Music Awards". Jamaa huyu kwanzia hapo alianza kutawala chart mbali mbali huko Jamaica akiwa na ngoma zake nyingine kama vile "Is There a Place","Beautiful Lady" na ile hit kali ya "Mama, Don't Cry".

Mwishoni mwa mwezi May 2010, ngoma yake ya "Hold you" ilichukua nafasi ya 91 kwenye chart za Billboard Hot 100, na namba 33 katika Billboard R&B/Hip-Hop Chart na namba 6 kwenye Billboard R&B/Hip-Hop Chart. Nyimbo hiyo ilizidi kupata umaarufu mkubwa pale alipoifanyia remix ambayo ndani alimshirikisha NickMinaj. Ambapo ngoma hiyo ilirudi tena katika chart za Billord nakuchukua namba 2.

Gyptian pia aliwika vilivyo na ngoma yake maarufu inayojulikana kwa jina la "Nah let go" ambapo ngoma hii ilitoka mnamo mwezi November mwaka huo huo, Ngoma hii ilijipatia umaarufu mkubwa mno UK na pande mbali mbali ulimwenguni.Gyptian aliachilia album yake Nothing to Lose mwaka 2015.

 
Gyptian amepata mafanikio makubwa mno katika muziki huu, amendika nyimbo nyingi mmno ambazo zinapendwa kote ulimwenguni. 'WINE UP' ndio ngoma nayoipenda mimi kutoka kwa jamaa huyu, je we unaipenda ipi kutoka kwa Gyptian?

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...