Klabu ya Manchester United
imeorodheshwa ya tano kwa utajiri duniani na jarida la Forbes, thamani
yao ikiwa imepanda kwa asilimia saba.
Klabu ya NFL, Dallas
Cowboys, ndiyo inayoongoza thamani yake ikiwa $4bn (£3.03bn), na ni mara
ya kwanza kwa klabu ambayo haichezi kandanda kuongoza katika orodha
hiyo tangu kuanzishwa kwake 2011.United, walioongoza orodha hiyo 2011 na 2012, wana thamani ya $3.32bn (£2.52bn).
Real Madrid ni wa pili kwa $3.65bn (£2.77bn) na Barcelona wa tatu $3.55bn (£2.69bn).
United, klabu pekee ya Uingereza katika orodha hiyo, walisaidiwa sana na mkataba wao wa £750m na Adidas, jambo lililoongeza thamani yao licha ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Hata hivyo, Manchester United, ndio wenye deni kubwa zaidi miongoni mwa klabu zilizo katika 25 bora.
Arsenal (23), Manchester City (28), Chelsea (36) na Liverpool (41) ndizo klabu hizo nyingine za Uingereza zilizofanikiwa kuwa kwenye orodha hiyo.
No comments:
Post a Comment