Thierry Henry ameondoka Arsenal, baada ya kukataa nafasi aliyopewa ya kufundisha wachezaji wa chini ya umri wa miaka 18.
Henry, 38, alipewa nafasi hiyo na meneja wa Arsenal, Arsene Wenger,
ambaye alimuambia kuwa hawezi kuchanganya na kazi yake ya sasa kama
mchambuzi wa soka kwenye TV.
Hata hivyo, Henry ambaye alifanya
kazi na wachezaji chipukizi wa Arsenal kama sehemu ya mafunzo ya kupata
leseni yake ya ukocha ya Uefa, hakuwa tayari kuacha kazi yake ya
uchambuzi wa soka.
Nahodha wa zamani wa Arsenal, Tony Adams, 49, sasa atachukua nafasi hiyo ya vijana chini ya miaka 18.
Henry sasa lazima atafute timu ya kufundisha ili kukamilisha leseni yake ya ukocha.
Thierry
Henry ameajiriwa na shirika la utangazaji la Sky Spors, na alifanya
kazi kama mchambuzi wa BBC wakati wa michuano ya Euro 2016.
12 July, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment