12 July, 2016

Tetesi za Soka Barani Ulaya

Chama cha soka cha England, FA, kitazungumza na meneja wa Hull City Steve Bruce, wakati wakiendelea na harakati za kutafuta meneja mpya wa England (Daily Telegraph), uhamisho wa Graziano Pelle kutoka Southampton kwenda Shandong Luneng ya China kunamfanya mshambuliaji huyo, 30, kuwa mchezaji wa sita anayelipwa zaidi duniani akipata pauni 260,000 kwa wiki (Sun).

PelleViungo Juan Mata, 28, na Bastian Schweinsteiger, 31, pamoja na mabeki Marcos Rojo na Daley Blind, 26, wanaonekana kama wachezaji wa ziada katika mipango ya meneja mpya wa Manchester United, Jose Mourinho (Daily Record), Villareal nao wamejiunga na Everton katika mbio za kumwania kiungo Juan Mata wa United (Daily Express).

BlindMeneja wa Manchester City Pep Guardiola anataka kumsajili beki wa Atletico Madrid, Lucas Hernandez, 20, kwa pauni milioni 20 (Sun), mshambuliaji kutoka Colombia, Marlon Moreno, 19, atasaini mkataba wa miaka mitano kwenda Man City, lakini atakwenda Deportivo La Coruna kwa mkopo msimu ujao (Daily Mirror), mwenyekiti wa West Ham, David Gill amesema klabu yake haitosikiliza dau lolote chini ya pauni milioni 50 kumtaka kiungo kutoka Ufaransa, Dimitri Payet, 29 (BBC Radio 5 Live).

PayetLazio wako tayari kumwacha Filipe Anderson, 23, kuondoka, huku Chelsea wakimtaka kiungo huyo (Gazzetta World), Chelsea pia wanataka kumsajili kiungo wa Barcelona, Arda Turan, 29, ambaye pia ananyatiwa na Arsenal (Sport), Chelsea vilevile wanajiandaa kutoa pauni milioni 34 kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon, Joao Mario 23 (A Bola).

GotzeLiverpool wamejitoa katika kutaka kumsajili kiungo wa Bayern Munich Mario Gotze, 24, huku Tottenham na Borussia Dortmund wakiendelea kumtaka (Liverpool Echo), kipa wa zamani wa Arsenal, Alex Manninger, 39, anafanya mazoezi na Liverpool akiwa na matumaini ya kupata mkataba (Sun), beki Martin Skirtel, 31, anatarajiwa kuwasili Istanbul kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 5.5 kutoka Liverpool kwenda Fernabahce (Daily Mirror).

SissokoEverton wamepanda dau la pauni milioni 25.5 kumtaka beki wa Juventus Daniel Rugani, 21 (Calcio Mercato), Christian Benteke, 25, hakaribii kuondoka Liverpool na kwenda Crystal Palace, kwa mujibu wa wakala wake (Evening Standard), Inter Milan wameweka bei ya pauni milioni 43, kwa klabu inayomtaka mshambuliaji wake Mauro Icardi, 23, ambaye anasakwa pia na Tottenham (AS), Newcastle watafikiria kumuuza kiungo Moussa Sissoko, 26, kwa timu itakayokuwa tayari kulipa pauni milioni 35 (Independent).

SOURCE: BBC

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...