11 May, 2016

Acha kuogopa maisha, Thubutu kufanya...

“Kuzaliwa Masikini Sio Kosa Lako, ila Kufa Masikini ni Kosa Lako Kubwa Sana”Msingi wa kufanikiwa ni kuthubutu kufanya jambo fulani kwa mfano kufungua miradi, kufanya biashara, kusoma kwa bidii na mambo mengine kibao.


Ngoja nikuulize tena, maana najua utakua ushaulizwa hili swali mara nying, Hivii unatamani kuishi au uwe kama nani ? wengi wetu mtasema natamani kuishi maisha mazuri na bora.


Hii iko hivi unapozungumza na watu wote duniani kila mtu atakwambia kuwa anataka kuwa na maisha mazuri ,huenda na ni vigumu kwa mtu wa kawaida kusema anataka maisha yake yawe ya shida kila siku. Huyo atakua ana lake.Wewe una stashahada una shahada na elimu nyingine nyingi, sijui umeahudhulia workshop kama ishirini, ila ndugu yangu bado utaendelea kuchapwa bakora na maisha kama hautakuwa makini na kuthubutu kufanya mambo unayotamani kufanya.


 Kusoma sana ama kidogo kuwa na marafiki waliofanikiwa ama wasiofanikiwa,kwenda nje ya nchi ama au kuzaliwa katika familia masikini au tajiri bado sio tiketi ya kukufanya uwe na maisha bora .


Kuna watu kwa mfano unaweza kuona anakata tamaa eti kisa amezaliwa katika familia maskini kitu ambacho sio sahihi.Bill Gates alisema “Kuzaliwa Masikini Sio Kosa Lako, ila Kufa Masikini ni Kosa Lako Kubwa Sana”


Yaani anamaanisha duniani kuna fursa nyingi sana ambazo unaweza kuzitumia na kuwa na maisha unayoyataka.


Kuwa na maisha bora ni kufanya kazi kwa bidii na  kwa malengo zaidi usiishi tuu ilimradi siku zinaenda mbele. Kwa chochote unachokifanya kifanye kwa kutafakari na kuangalia faida na hasara yake.

Yapo mambo mengi ambayo yameweza kuzungumzwa ambayo yanaweza kukusababishia wewe kusonga mbele kimaisha lakini hata ukisoma mambo mengi yanayohusu mambo ya kimaisha bila kuthubutu kufanya kitu unachotaka kufanya ni kazi bure.


 Inabidi kuwatathimini watu ambao wanakuzunguka, kuanzia marafiki, majirani, na hata baadhi ya ndugu.Kuna wengine hata ukimwangalia sura yake tu anaonekana wazi kuwa hana furaha unapomwambia kuwa mambo yako yanakwenda vizuri kwa sababu watu wengi wanapenda kusikia kuwa unaishi maisha ya shida ndio wengi walivyo na wakijua hivyo ndio unaongeza uoga wa kuthubutu kufanya kazi. Sijui kwa nini hii inatokea, lakini achana na hao wewe kazana kubuni miradi mingi ili uwe na maendeleo bora maana wao kukasirika haikuzuii kufanya mambo yako.


Mafanikio yako yanatokana na akili yako ulionayo maana wengine wamekuwa wakisema kuwa ugumu wa maisha ndio kipimo chako cha akili yako.


Katika jamii tunakoishi utakua ushasikia watu wanalalamika kuwa maisha ni magumu,na hawajui wafanyaje lakini nikwambie kuwa kipimo cha maisha unacho hapo wewe mwenyewe na akili yako. Kama unajua kusoma na kuandika ni tosha kabisa kwa wewe kujiendeleza.


Kwaiyo jamani ni vizuri ukakaa na kutathimini unatamani maisha yako yaweje au unataka kuishi vipi  au maisha yako yakae katika level gani ya kimaisha hapa duniani? Kipimo cha maisha ambayo unataka  kuishi unacho wewe mwenyewe pia uoga wako ndo umaskini wako yawezekana hapo ulipo kaa una wasiwasi ,una uoga ,unawaza una tathimini wakati nguvu unazo, sababu unazo, elimu unayo vifaa pia unavyo. Ila… kwa kumalizia Kitu kimoja tu unahitaji ndugu yangu. “JITUME”.


Ukitaka kuelewa hii angalia wiki nzima iliyopita kama umefanya kitu ambacho kinaendana na mambo ambayo unataka kufaninikiwa maishani mwako. Kama kipo Good… kama hakipo, basi anza kujituma leo… yaani leo namaanisha anza kupanga mikakati, kama serikali inavyoweka mipango na mikakati ya miradi yake kwa wananchi na wewe kaa chini tengeneza mikakati ya maisha yako.


Kumbuka Unapanga mikakati ya maisha YAKO! Sio ya jirani yako ambae anakusema sema kila siku au mlie kosana nae juzi.


PITIA NA HIZI PIA

   >>> Tuzungumze yanayo tusibu na Kupata suluhisho.

  >>>  Viashiria 6 ni kwa nini unatakiwa kubadili Maisha yako Leo.  

 >>>    Furaha ya kweli inaletwa na wewe mwenyewe.Je ungependa kupokea Makala na Mafundisho yangu kila ifikapo Week End Bure? Jiunge leo na watu 3000 waliochagua kupokea Makala zangu kila Week End Bure kupitia Email!

* Inahitajika

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...