Mkufunzi wa kilabu ya Chelsea Jose
Mourinho amesema kuwa kinyang'anyiro cha kuwania ubingwa wa ligi ya EPL
bado kiko wazi licha ya timu yake kuwa mbele na pointi saba mbali na
mechi moja ambayo haijacheza.
Mourinho anaamini kuwa timu yoyote
ambayo iko nyuma na pointi saba ama nane bado ipo katika kinyang'anyiro
na kwamba hashangazwi na kushuka kwa Manchester City katika kupigania
taji hilo.Chelsea itamenyana na QPR ugenini jumapili katika debi ya Magharibi mwa London.
No comments:
Post a Comment