Klabu ya soka ya
Manchester United haitotakiwa kuibeza Manchester City kutokana na
matokeo ya siku za mwisho kwao kutokuwa mazuri, na hili alisema Van
Gaal.
Kikosi cha mashetani
hao wekundu maarufu kwa jina la Red Devils wapo katika maandalizi ya
Jumapili kuikabili City kufuatia ushindi mzuri mzuri walioupata siku ya
jumamosi dhidi ya Aston Villa wa goli 3-1.
Msimu huu kwa City
umekuwa sio mzuri kwao mara baada ya kushindwa kufurukuta katika mechi
yao ya mwisho ya ligi kuu kwa kuchapwa na Crystal Palace wakiwa ugenini
wa goli 2-1 na kuanza kupoteza matumaini ya kutetea taji la ligi hiyo
kama mabingwa watetezi.
Van Gaal amesema aina
ya uchezaji wanaocheza City huwa unaleta taabu kwao kutokana na
utofauti wa vikosi vyao na hivyo hawana budi kupambana zaidi ili waweze
kuendelea kubakia katika nafasi yao ya 3.
” Villa walitumia
mfumo wa kujilinda sana lakini sitarajii kwa Manchester City kufanya
vile kama Villa walivyotufanyia na pia inahitaji kuwa na ulinzi makini
zaidi kwetu” Van Gaal alisema.
” Jumapili tubasubiri
tuone kama tunaweza kuendeleza kiwango chetu cha ushindi dhidi ya
Manchester Unity” Van Gaal aliongea na Goal.com
Katika raundi ya
kwanza ya ligi kuu City walifanikiwa kuifunga United kwa bao 1-0 ambalo
lilifungwa na Kun Arguero huku Chris Smalling akienda nje baada ya
kupata kadi nyekundu ambapo ilikuwa ni mwezi wa 11.
Van Gaal hakusita pia kuongelea umakini wa wachezaji uwanjani pia akazungumzia ile kadi aliyopata Smalling.
” Mara kwa mara
nimekuwa nikilizungumzia hili na katika mechi ya aina kama hizi hatuna
budi kuongoza zaidi fikra zetu, tuna kadi 5 nyekundu na hili halijawahi
kutokea katika kazi yangu, ni historia” Van Gaal alisema
No comments:
Post a Comment