11 April, 2015

Real Madrid wamecheza leo Elbar


Ligi kuu ya Hispania imeendelea tena jioni ya leo – huku Real Madrid na Elbar wakifungua pazia la mechi za leo.
Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo  ameziteka tena ‘headlines’ za vyombo vya habari baada ya leo kuiongoza timu yake kupata ushindi wa magoli 3-0.

Ronaldo alifungua akaunti yake ya magoli leo kwa mkwaju wa adhabu ndogo katika dakika ya 21 ya mchezo huo – goli la leo limemfanya Ronaldo atimize magoli 38 katika La Liga msimu huu. Goli hilo lilotokana na mkwaju wa adhabu ndogo ni la kwanza tangu Ronaldo alipofunga goli dhidi ya Bayern Munich katika nusu fainali ya Champions League takribani miezi 12 iliyopita. Magoli mengine ya mchezo huo yalifungwa na Javier Hernandez Chicharito dakika ya 31 na Jesse akamalizia kazi kwa goli zuri dakika ya 83.
FC Barcelona wanaongoza ligi ya Spain wanacheza na Sevilla usiku huu.


Mawerenewz.blogpot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO,SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA
Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Francis mawere the jr, Instagram>>>Zawadi_mawere. AKSANTE.

              
          

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...