NIPASHE
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mussa Lupatu ni miongoni mwa waliofariki katika ajali ya mabasi mawili na gari ndogo iliyotokea kijiji cha Mkata Tanga.
Kaimu Kamanda wa Polisi Tanga, Juma Ndaki amesema Marehemu Lupatu
alipata ajali hiyo akitokea Kibaha kuelekea Korogwe kumpeleka mwanae
kupatiwa matibabu ya ugonjwa akili ambaye naye pia alifariki.
Wengine waliyotajwa kufariki katika
ajali hiyo ni karani wa Mahakama ya Ardhi Dar es Salaam, Devota Msimbe
ambaye alifariki wakati akikimbizwa Hospitali ya Muhimbili.
Kamanda Ndaki alisema
maiti tatu bado hazijatambuliwa na miili yao imehifadhiwa katika
hospitali ya Magunga Korogwe, majeruhi 12 bado wamelazwa katika
Hospitali tofauti.
Majeruhi 12 kati ya 34 wamelazwa katika
hospitali tofauti, wakiwamo saba waliopelekwa Muhimbili, mmoja hospitali
ya wilaya ya Handeni na wanne kituo cha afya Mkata, wilayani Handeni.
NIPASHE
Watu wanaoishi Vigwaza, wilaya ya
Bagamoyo wameamua kuwaajiri watoto wao waliomaliza kidato cha nne
kufundisha Shule ya Msingi Visezi, ili kutatua tatizo la upungufu wa
walimu shuleni hapo huku wakiwalipa posho ya sh. 15,000 kwa wiki.
Wananchi hao wamesema wanawalipa watoto hao Sh. 15, 000 kwa wiki kama posho ya kujikimu.
Walisema wameamua kuajiri watoto wao
baada ya kuona wamekuwa na changamoto hiyo kwa aidi ya miaka 10 na
hakuna juhudi zozote zinazofanywa na serikali kutatua tatizo hilo.
“Ngoja
tukwambie, sisi wanavisezi wote ni wanaCCM kwa hiyo usiwe na wasiwasi
lakini kama hutatatua hizi kero zetu CCM itashinda kwa shida sana, sio
siri,”—alisema Mwenyekiti wa kijiji hicho, Hamisi Kiatala.
“Kero ya walimu itakwisha hivi
karibuni.. TAMISEMI wana mpango wa kuwaajiri walimu, lakini viongozi wa
kijiji hamjawahi kuniambia hizi kero zenu wakati mimi ni mbunge wenu pia
ndio waziri mwenye dhamana… hizi kero zinazowezekana kutatua
nitazitatua kwa kushirikiana na viongozi wa kijiji, zitakazoshindikana
tutazishughulikia mwakani kama nitarudi tena”, alisema Kiatala.
HABARI LEO
Kusambaa kwa taarifa kuwa kuna uwezekano
wa kutokea kwa shambulio la kigaidi katika miji ikiwemo Dar na Mwanza
kumefanya baadhi ya Taasisi kama vyuo vikuu na TANESCo kuchukua
tahadhari kwa kuweka taarifa ya tahadhari na kuelekeza namna hatua za
kufanya ili kujiepusha na kujilinda.
“Kutokana
na tishio hilo, tumeona ni vyema tuchukue hatua mapema.. si lazima
yatokee ndivyo tuchukue hatua, tumeona ni vyema kujihami kwa kuimarisha
ulinzi katika vituo vyetu..”—Mkurugenzi wa TANESCo, Felchesmi Mramba.
Baadhi ya tahadhari walizozichukua
Taasisi hizo ni wafanyakazi na wanafunzi kuvaa vitambulisho vyao wakati
wote, ukaguzi wa wageni na watu wote wanoingia maeneo ya Taasisi hizo,
pamoja na kuwekwa kwa matangazo ya tahadhari katika maeneo hayo.
Jeshi la Polisi limeonywa watu kuacha
tabia ya kutunga na kusamba ujumbe kwenye simu na mitandao ya kijamii
unaowatia hofu wananchi.
No comments:
Post a Comment