11 April, 2015

Coastal ilijiweka katika mazingira magumu ya kuboromoka

coastal-unionCoastal ilijiweka katika mazingira magumu ya kuboromoka daraja baada ya kuruhusu kufungwa idadi kubwa ya mabao 8-0 dhidi ya Yanga Jumatano.’
BAADA ya kupigwa 8-0 dhidi ya Yanga SC Jumatano, Coastal Union FC imezindukia Chamazi, Mbande jijini hapa ikikichapa kikosi cha JKT Ruvu Stars mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Bara iliyochezwa jioni hii Uwanja wa Azam.

Kwa ushindi huo, kikosi cha kocha wa zamani wa Simba SC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye muda wowote atawekwa pembeni ya timu ya Wagosi wa Kaya, kimepanda kutoka nafasi ya 11 hadi nafasi ya sita kikifikisha pointi 27 baada ya mechi 23.
Ikiwa ni kawaida yake ya kutofanya makosa katika mikwaju ya penalti, mshambuliaji Mkenya Rama Salim aliipatia Coastal bao la kwanza katika dakika ya 10, bao ambalo limedumu kwa kipindi chote cha kwanza.
Licha ya vijana wa JKT Ruvu Stars wanaonolewa na kocha wa zamani wa Yanga SC, Fred Felix Minziro, kilifanya mashambulizi mengi langoni mwa Wagosi wa Kaya, lakini hakikufanikiwa kupata bao la kusawazisha kisha kujikuta kikiongezwa bao la pili na kukinyong’onyesha kabisa.
Bao hilo limefungwa na mshambuliaji wa kimataifa Ike Bright Obina katika dakika ya 83 baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa wenyeji.
Kwa matokeo hayo, kikosi cha Minziro kimeshuka kwa nafasi moja kutoka nafasi ya nane hadi ya tisa katika msimamo wa ligi kikiendelea kubaki na pointi zake 24 baada ya mechi 22.
Katika hatua nyingine, mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar FC na wageni Ruvu Shooting Stars haikuchezwa leo jioni Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga kutokana na mvua kubwa.
Kocha mkuu wa Kagera Sugar FC, Jackson Mayanja na msemaji wa Ruvu Shooting Stars, Masau Bwire, wameaumbia mtandao huu muda mfupi uliopita kuwa wamekubaliana mechi hiyo ichezwe Jumatatu jioni.
Ni mara ya pili msimu huu mechi kuahirishwa kwenye uwanja huo msimu huu baada ya wiki iliyopita mechi ya Kagera Sugar FC dhidi ya Simba SC kuchezwa Jumatatu alasiri ya wiki hii badala ya Jumamosi jioni ya wiki iliyopita.
Matokeo mengine ya Ligi Kuu Bara leo ni kama ifuatavyo:
Mtibwa    1-1    Azam
Ndanda    0-0    Prisons
KESHO
Yanga    ?-?        Mbeya City
Stand    ?-?    Polisi Moro



Mawerenewz.blogpot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO,SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA
Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Francis mawere the jr, Instagram>>>Zawadi_mawere. AKSANTE.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...