04 April, 2015

Kumbe Habida aliwahi kubakwa? ilikuaje? na anaichukuliaje sasa hivi?




Tulilijua kwa ukubwa jina la Habida baada
ya kutoa hit single ya kesho zaidi ya miaka mitano iliyopita akiwa ni
mwimbaji kutokea Kenya.


Kwenye interview na show ya Mambo Mseto ya
Radio Citizen Kenya, kwa mara ya kwanza Habida amefungua kinywa chake na
kukiri aliwahi kubakwa akiwa mdogo.
Ilitokeajie???? >>>>>> ‘Nilikua
bikra wakati huo na huyo Mwanaume alikua akisema wewe nitakupata tu,
sasa siku moja ilitokea nikawa nimetoka na marafiki zangu, nikalewa na
wakati nataka kwenda nyumbani huyu Mwanaume akasema atanipeleka nyumbani
lakini hakunifikisha, ndio akanibaka
Kwenye sentensi nyingine, Habida amesema
anataka kuwaonyesha Wanawake wengine kwamba hata kama ukibakwa
haimaanishi ndio umefeli maisha, anataka kutumia kilichomtokea kuonyesha
Wanawake wengine kwamba hata kama kuna kitu kilitokea hakikuharibu
maisha yake, yuko hapa na ameendelea na maisha, single yake mpya inaitwa
Keep on walking.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...