Maabingwa wa zamani wa ligi kuu
ya Tanzania bara, ambao ni wawakirishi pekee wa Tanzania katika michuano
ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Dar es Salaam Young Africans, leo
wamefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo
licha ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya FC Platinum.
Yanga ambao walikuwa na faida ya
bao 5 ambazo walizipata katika mchezo wa kwanza uliopigwa Jijini Dar Es
Salaam wiki mbili zilizopita, leo walijikuta wakifungwa na wenyeji hao
kupitia kwa W. Musona kunako dakika ya 30 kipindi cha kwanza kwa shuti
kali akiunganisha krosi safi kutoka upande wa kushoto.
Katika mchezo huo Platinum
walikuwa wakishambuia kwa wingi lango la Yanga huku Watanzania hao
wakifanya mashambulizi ya Kushitukiza, ambapo dakika ya 4 Platinum
Walipata bao lakini muamuzi akalikataa kwasababu tayari mchezaji alikuwa
amekwisha otea.
Dakika ya 12 Kipa wa Yanga Ally
Mustafa Bartez aliisaidia Yanga baada ya kuokoa mchomo uliopigwa langoni
huku mshambuliaji wa Platinum akiwa na kipa lakini kipa huyo akapangua
na kufanya Yanga waanze upya kujipanga.
Mshambuliaji wa Yanga Mrisho
Halfani Ngassa alikosa bao kunako dakika ya 22 baada ya ‘kukunjuka,
kupiga Tik-Tak ambayo haikuzaa matunda kufatia kichwa cha Amis Tambwe
aliyeunganisha mpira wa kona uliopigwa na Simon Msuva.
Hadi muamuzi anapuliza kipenga
cha mwisho kuashiria kipindi cha kwanza kimemalizika Yanga walikuwa
Nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Musona.
Kipindi cha pili kilianza kwa
kasi ambapo kocha wa Yanga Hans Van Pluijm aliamua kumtoa beki Said Juma
Allly na nafasi yake akaingia mkongwe Calvin Yondani ili kuhakikisha
Platinum hawapati bao linguine na kuwaweka Yanga katika wakati mgumu.
Dakika ya 53 Mrisho Ngassa
anakosa bao la wazi baada ya kupenyezewa pasi na Kiungo Haruna Niyonzima
lakini Uncle akawa kwenye kizingiti cha mabeki wa Platinum ambao
waliokoa mpira huo.
Simon Msuva kunako dakika ya 55
aliwakosesha Yanga bao baada ya kuwaadaa mabeki wa Platinum na kuachia
shuti kali ambalo pia halilkuleta madhara na kugeuka mboga kwa kipa wa
Platinum.
Ili kuhakikisha labda wanapata
angalau bao la ugenini hata moja Kocha Hans Van Pluijm aliamua
kumpumzisha Msuva na nafasi yake kuchukuliwa na Dan Mrwanda kunako
dakika ya 89.
Baada ya dakika 4 za nyongeza
Mrisho ngasa alipewa kadi ya Njano kwa kumchezea vibaya mchezaji wa
Platinum ikiwa ni pamoja na kupinga maamuzi ya Refa.
Hadi dakika ya mwisho Yanga
wanauwa wamefanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5 kwa 2 kwani
mchezo wa awali matokeo ilikuwa 5 kwa Yanga na 1 kwa Platinum.
No comments:
Post a Comment