Ligi kuu ya Uingereza jioni ya leo imeendelea katika viwanja tofauti nchini humo huku Arsenal ‘The Gunners’ wakiwafumua Liverpool kwa jumla ya mabao 4-1 na kufanya ndoto wa Majogoo hao wa jiji la Landon kuzidi kupoteza matumaini ya kushiriki klabu bingwa Ulaya mwakani.
Arsenal ndio walianza kupata bao
kupitia kwa Hector Bellerin kunako dakika ya 37 kabla ya Ozil kucheka na
nyavu dakika ya 40 baada ya kuachia shuti kali lililotokana na adhabu
ndogo kufatia mchezaji wa Aresenal kufanyiwa madhambi.
Dakika ya 45 Sanchez aliiandikia
The Gunners bao la tatu kabla ya Olivier Giroud kufunga kabisa idadi
ya mabao katika uwanja wa Emirates kwa kuandika bao la 4, Bao pekee la
Liverpool limefungwa na Jordan Henderson kwa mkwaju wa penati.
Katika mchezo huo Mchezaji wa
Arsenal ambao walikuwa wanatumia mfumo wa (4-2-3-1) na Timu ya Taifa ya
Ujerumani, Mesut Ozil, alifanikiwa kuibuka
Man of the Match.Kocha wa Arsenal
Mfaransa Arsene Wenger aliwatumia Ospina, Bellerin, Mertesacker,
Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla, Ramsey, Sanchez, Ozil, Giroud. huku wengine wakianza benchi kama, Gibbs, Macey, Rosicky, Walcott, Welbeck, Gabriel, na Flamini.
Kikosi cha Liverpool kikiwa chini ya Brendan Rodgers ambacho kilitumia mfumo wa
3-4-2-1 kilikuwa ni Mignolet, Can 5, Toure, Sakho, Henderson, Allen,
Lucas, Moreno, Markovic, Coutinho, Sterling huku Sturridge, Borini,
Brannagan, Johnson, Jones, Lovren, Manquillo wakianzia benchi.
Kuatia matokeo hayo sasa Aresenal inakuwa imeishusha
Manchestar City katika nafasi ya pili ikiwa na alama 63 mele kwa pointi 2
huku wakiendelea kusoma namba za Chelsea wanaoongoza kwa alama 67.
No comments:
Post a Comment