KIONGOZI wa juu wa Shirikisho
la soka nchini Morocco, Nour Eldin Boushehati ameweka wazi kuwa taifa
lake liko tayari kuwa mwenyeji wa fainali za mataifa ya Africa, Afcon
2017.
Mahakama ya juu ya rufani ya
FIFA ya masuala ya mpira (CAS) alhamisi ya wiki hii iliitangaza Morocco
kuwa huru kutoka katika kifungo cha CAF na kusema wanaweza kushiriki
fainali za Afcon 2017 na 2019.
Boushehati sasa anajiamni kuwa wako tayari kuhodhi michuano hiyo kwa miaka miwili mfululizo.
“Tuko yatari kuwa wenyeji wa
michuano ijayo ya Afcon kama serikali itatupa ruksa, tuko tayari,
tunaisikiliza serikali. Wakituruhusu tutakuwa tayari kuwa wenyeji,”
Amesema Boushehati.
Morocco walitakiwa kuwa wenyeji
wa fainali za Afcon mwaka huu 2015 lakini walichomoa dakika za mwisho
wakihofia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Guinea ya Ikweta ilikubali kuwa mwenyeji wa fainali hizo muda mfupi baada ya kuombwa na CAF.
No comments:
Post a Comment