15 October, 2015

Kisa cha Santos kutaka Neymar afungiwe miezi 6 hiki hapa

Klabu ya Santos ya Brazil imeripotiwa kutuma maombi FIFA imfungie miezi sita mchezaji wao wa zamani Neymar kwa miezi 6 kama sehemu mambo yao ya kisheria dhidi ya mshambuliaji huyo na klabu yake mpya ya FC Barcelona.
  Kwa mujibu wa Sport, Santos wanahisi kusalitiwa na nahodha wa Brazil ambaye kwa mujibu wao alikiuka mkataba baina yao alipojiunga na Barca mwaka 2013. Pia inasemekana wanataka malipo ya fidia ua kiasi cha €55million katika adhabu ambayo wanataka FIFA itoe.
Haijafahamika lini FIFA itatoa maamuzi katika kesi ya Santos dhidi ya Neymar ya kutaka shirikisho hilo limfungie kwa miezi 6.
  Mashtaka ya Santos’ yanaelezea katika toleo la gazeti la Sport: “Neymar anatuhumiwa na Santos kuvunja kanuni namba 63 ya nidhamu. Katika jalada lao la mashtaka pia Santos wamezungumzka namna mchezaji alivyokosa utii wa sheria za uhamisho za FIFA za namba 17(3) and 17(5).”
Neymar amekanusha kuvunja sheria/kanuni yoyote kama anavyotuhumiwa na waajiri wake wa zamani, akisisitiza alihamia Barcelona mara tu baada ya kukubaliana kimsingi na Santos. Kwa mujibu gazeti la Sport, Neymar ana barua ya kutoka kwa Raisi wa Santia Luis Alvaro de Oliveira ambayp ilikuwa inampa ruhusa ya kuanza kuzungumza na Barcelona.
Santos walitangaza kwamba wangemchukulia hatua mchezaji wao wa zamani, baba yake Neymar na Barcelona mwanzoni mwa mwaka huu, wakiwatuhumu kufanya udanganyifu katika majadiliano ya uhamisho wa Neymar. Santos wanasema Barca walifanya udanganyifu katika malipo halisi ya waliyolipa na waliyoyatangaza.
  Ada waliyoripotiwa kulipa Barcelona mwanzoni kwa ajili ya Neymar ilikuwa €57 million (£42 million), lakini uchunguzi wa baadae ulionyesha bei halisi ni €86.2 million (£63.5 million).
Mpaka sasa Raisi wa zamani wa Barca Sandro Rossell na wa sasa Joseph Maria Bartomeu wana kesi mahakamani juu ya udanganyifu huu.

Kizza Besigye akamatwa Uganda


Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda, Kizza Besigye amekamatwa pamoja na wanachama wengine wa chama chake.
Kukamatwa kwao kunajiri wakati ambapo chama hicho kilikuwa kinaanza kampeni zake kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao kulingana na mwandishi wa BBC Patience Atuhaire katika mji mkuu wa Kampala.
Watu wengine wawili pia walikamatwa pamoja na bwana Besigye wakati maafisa wa polisi walipovamia nyumba yake mapema leo kulingana na vyombo vya habari.
Mbunge wa chama hicho Ssemujju Nganda ambaye pia ni msemaji wa chama hicho pia alikamatwa nyumbani kwake na amepelekwa katika kituo cha polisi cha Naggalama,karibu na mji mkuu wa Kampala.
Besigye amepoteza mara tatu kwa rais Yoweri Museveni katika uchaguzi uliokumbwa na utata.

Upinzani wapinga matokeo ya uchaguzi Guinea


Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Guinea amejiondoa katika uchaguzi uliofanyika nchini humo akisema kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa uliotekelezwa na serikali kulingana na kiongozi wake wa kampeni.
Uamuzi huo wa Cellou Diallo wa kujiondoa unajiri wakati ambapo matokeo yanaonyesha kwamba rais Alpha Conde anaongoza kwa wingi wa kura akitafuta kushinda awamu ya pili ya miaka mitano.
Wachunguzi kutoka muungano wa Ulaya wanasema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki licha ya matatizo makubwa ya vifaa.
Matokeo kamili ya uchaguzi huo yanatarajiwa mwishoni mwa wiki hii.

Lil wayne ajichanganya baada ya Lamar Odom kuzidiwa, aandika ‘R.I.P’

Mchezaji wa zamani wa timu ya kikapu ‘LA Lakers’ na mume wa zamani wa Khole kardashian, Lamar Odom yupo hoi kitandani baada ya kudaiwa kutumia kiwango kikubwa cha dawa za kulevya Cocain kiasi cha kupaatwa na kiharusi na figo zake kushindwa kufanya kazi.Lil wayne ni mmoja ya mastaa wakubwa waliopokea habari hiyo tofauti na ukweli halisi, alitweet “R.I.P LO,Dam man. My blessings to ur fam and friends.” lakini baada ya muda aligindua kuwa alikua amejichanganya, na kuwa mcheza kikapu huyo bado yupo hai, Alitweet tena  “Woop.”

Vyanzo mbalimbali vimedai kuwa Odom aliamua kubwia unga kwa kiasi kikubwa baada ya kupokea simu iliyomuudhi inayohusiana uhusika wake kwenye show ya Keeping up with the Kardashians hata hivyo wanafamilia hao wa The kardashians walifika Hospitalini hapo kumjulia hali.

I am The Black Gold of the Sun


These are random picks of pictures i came across today and had to share

 Celebrate the Black Gold in you,everyday...because You and I ARE the Black Gold of the Sun
Pictures from Arteide's Album on The Human Race

Huu hapa mchongo mpya wa P.diddy..kuanzisha kipindi cha Comedy kinachohusiana na Maisha ya kweli ya Msaidizi wake


Rapper, Producer, Muigizaji na mjasiliamali Sean Combs amejiunga na kituo cha runinga cha ABC kuandaa kipindi cha vichekesho kitakachohusu maisha ya kweli ya aliyekua msaidizi wake Sarah Snedeker.
Kipindi icho cha Vichekesho  ambacho kitarekodiwa na kamera moja tu tayari kimeandikiwa Script kitaonesha maisha ya binti aliyetoka kwenye maisha duni lakini anapata bahati ya kuwa msaidizi wa Billionaire mkubwa lakini anajikuta akiangukia kwenye maisha machafu ya ubadhirifu na ufisadi na vitu vingi vinavyomsahaulisha alipotoka.

Ulishawahi kujiuliza kuna maneno gani mengine ya kumwambia mpenzi wako tofauti na ‘I love you’ ?


‘Nakupenda’ ni  neno tamu ambalo unaweza mwambia  hivyo  mpenzi wako mara kwa mara lakini si neno pekee ambalo watu wengi wanapenda kusikia mara kwa mara. Yapo mambo mengi ya kumwambia mpenzi wako apate amani, hii inajenga upendo na  Heshima kati yenu.
  1. Mwambie Anaweza:
Kuna wakati tunapitia mambo magumu sana katika maisha na watu wanakata tamaa ya maisha wanakosa uthubutu wa kujaribu tena na tena, kama amefeli mtihani,amepata ajari ya gari, amepata hasara ya kibiashara mwambie “baby you can” mwambie anaweza kuendelea na maisha yataendeleea mtie moyo hii itamfanya ajiamini na kuona thamani yake kwako.

  1. Unanivutia
Mwambie ni kiasi gani anakuvutia, mwambie alivyo mrembo/mtanashati  mueleze ni kiasi gani unakuwa  na furaha akiwa karibu nawe, hii itamsaidia mpenzi wako kujiamini.  Msifie mpenzi wako  kwa suti au tai yake mpya , msifie msichana  kwa kiatu chake na gauni lake zuri kabla hajatoka nyumbani sababu anaweza akasifiwa na wengine, kwahiyo kuwa wa kwanza kumpa sifa hizo atajisikia wa fahari.

  1. Unajivunia kuwa Nae
Mambo yanaweza yasiwe vile mnavyotaka wakati wote, kuwa karibu na mwenza wako  na umuelezee ni kwa kiasi gani unajivunia kuwa nae, nafasi yake katika maisha yako na umuhimu wake ni faraja kwako, mueleze na umuonyeshe pia matendo yanaongea zaidi ya maneno.  Mwambie “am proud of you”

  1. Omba Kutoka Nae.
“Let’s go out”  hapa wasichana wengi huwa wanasubiri watoke na wapenzi wao mpaka waambiwe au mpaka mpenzi wake apange kutoka nae, chukua nafasi ya kumtoa  mpenzi wako mara moja moja na ugharamie huduma zote za siku hiyo, kama ni safari ufukweni, hotelini au migahawa mjini. Kama msichana kuwa tofauti na wale wasichana wanaosubiri kila siku ofa za mpenzi, kuwa tofauti usisubiri mpenzi wako akutoe, mtoe wewe siku moja.

  1. Msamaha
Uwe mwepesi wa kusema neno samahani kila mara, kuna kukoseana mara kwa mara kuwa wa kwanza kuomba msahama hii itapunguza hasira za mapenzi wako na malumbano pia hayatapata nafasi, hii itasaidia kuhimarisha mahusiano ya muda mrefu.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...