10 August, 2015

BAADA YA KUCHIMBWA MKWARA NA MOURINHO, DAKTARI WA CHELSEA ATOA NENO KWA MASHABIKI

Carneiro
Daktari wa Chelse Eva Carneiro amewashukuru mashabiki waliomtia moyo baada ya kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho kuishambulia timu ya matabibu akisema kwamba ni ‘wajinga’.
Katika sare ya goli 2-2 dhidi ya Swansea kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya England, Mourinho alichukizwa na kitendo cha Carneiro kuingia uwanjani kumtibu Eden Hazard na kutumia muda mrefu ilihali dakika zikiwa zimesalia chache.
Chelsea doctor Eva Carneiro thanks fans for support after Jose Mourinho lays into his
Wakati huo Chelsea walilazimika kubaki 9 uwanjani na Swansea wakapata fursa ya kulisakama lango la Chelsea.
Mourinho alisema daktari huyo hakuelewa mchezo.
Carneiro amesema: “Napenda kuwashukuru watu wote walionipa moyo. Kiukweli nimepata faraja sana”.
The Chelsea doctor tends to be private but she posted on Facebook to thank those backing her judgement

TWIGA STARS YAENDELEA KUKAMUA MAZOEZI ZANZIBAR

Twiga mazoeziniKikosi cha timu ya timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa Amaan na uwanja wa Mafunzo vilivyopo kisiwani Zanzibar.
Twiga Stars iko kambini visiwani Zanzibar kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofanyika nchini Congo- Brazzavile kuanzia Septemba 04–19 mwaka huu.
Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage ameendelea kukinoa kikosi chake cha wachezaji 25 waliopo kambini visiwani Zanzibar kujiandaa na michuano hiyo ya Afrika.
Twiga Stars itakua kambini kwa kipindi cha mwezi mmoja, kujiandaa na fainali hizo za michezo ya Afrika, ambapo imepangwa kundi A pamoja na wenyeji Congo-Brazzavile, Ivory Coast na Nigeria.

Watu 10 wauawa katika mkanyagano India


Takriban watu 10 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika mkanyagano uliofanyika katika hekalu moja katika jimbo la mashariki la Jharkhand nchini India .
Mahujaji wamekuwa wakiadhimisha sherehe ya kidini ya Hindu katika mji wa Deoghar.
Kisa hicho kilitokea wakati mahujaji walipokuwa wakiingia ndani ya ukumbi huo.
Mikanyagano mibaya hutokea mara kwa mara nchini India wakati wanapoadhimisha sherehe za kidini ambazo huvutia makundi makubwa ya watu bila ya kutilia maanani usalama.
Mkanyagano huo katika hekalu la Baidyanath Jyotilinga ulianza baada ya mahujaji kuelekea eneo takatifu mda mfupi baada ya milango kufunguliwa siku ya jumatatu.

Weusi 2 wapigwa risasi Ferguson,Marekani


Mtu mmoja amejeruhiwa vibaya huko Ferguson, Missouri, huko Marekani baada ya kisa cha ufyatulianaji risasi uliotokea katika dakika za mwisho mwisho za maandamano ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuuawa kwa mvulana mweusi Michael Brown na polisi mwaka uliopita.
Kisa hicho cha mauaji kilisababisha mtafaruk baina ya watu wa jamii ya wamarekani weusi na polisi.
Barubaru huyo tayari amefanyiwa upasuaji na anasemekana hali yake ya afya imedhibitiwa kwa mujibu wa polisi.
Polisi wanasema kuwa walikuwa wakimsaka barubaru huyo kwa kipindi kirefu baada ya kupokea habari kuwa alikuwa amejihami kwa bunduki iliyoibwa.
Jina la mhasiriwa huyo halijajulikana kufikia sasa.
Mkuu wa polisi katika jimbo hilo la Ferguson Jon Belmar amesema kuwa tayari maafisa 4 wa polisi wamehssimamishwa kazi ilikufanikisha uchunguzi wa kina kuhusu kisa hicho.
Picha kutoka eneo la tukio zinaonesha mtu mweusi anayetokwa na damu akiwa amelala sakafuni.
Awali,mamia ya watu walisimama kimya kwa muda wa dakika nne na nusu kwa pamoja mjini Ferguson ,Missouri katika sehemu ile ile ambayo kijana asiye na hatia Michael Brown aliuwawa na polisi mmoja wa kizungu mwaka mmoja uliopita.
Ishara hiyo inaashiria muda ambao mwili wake ulilala katikati ya barabara bila kupata msaada wowote.
Njiwa wawili walipeperushwa hewani na watu waliandamana kimya kimya ili kutoa heshima kwa Michael Brown na wengine ambao walikufa katika mikono ya polisi.
Mauaji hayo yalileta mjadala dhidi ya ubaguzi wa polisi nchini Marekani na ulimwenguni.

Wahubiri wa TZ waliotekwa kuwachiliwa

Mtu anayeongoza mazungumzo ya kuachiliwa huru kwa wahubiri saba wa kiislamu kutoka Tanzania waliotekwa nyara wiki iliopita ameiambia BBC kwamba makubaliano ya kuwaachilia huru huenda yakaafikiwa hivi karibuni.
Sheikh Suleiman Mohammed amesema kuwa kundi la watu wanaofanya mazungumzo hayo limewasiliana na watekaji nyara hao na kwamba viongozi hao wa dini hawajateswa.
''Wametaka kupewa fedha ili kuwahudumia mateka hao iwapo fedha za fidia hazitalipwa'',aliambia BBCswahili.
Ameongezea kuwa maimamu hao sio waliokuwa wakilengwa na washambuliaji hao na kwamba walikuwa katika mahala pabaya katika wakati usiofaa.

Ugonjwa wa sukari ni chimbuko la chakula kisichofaa

Ni vigumu kujua aina ya chakula kinachokufaa, bila kujua jinsi mwili wako unavyokichakata. Kimsingi watafiti wamebaini makundi makuu matatu ya watu kuhusiana na jinsi miili inavyochakata chakula.

Chakula ambacho ni bora kwa mtu mmoja, kinaweza kuwa sumu baridi kwa mtu mwingine na kumletea madhara endelevu katika maisha yake. Kwa muktadha huu basi hakuna chakula bora kwa kila mtu. Chakula ni bora kwa mtu kama baada ya kukitumia mwili utakipokea vizuri, ukafyonza virutubisho na kikasaidia kuimarisha afya ya mlaji.

Ni vigumu kujua aina ya chakula kinachokufaa, bila kujua jinsi mwili wako unavyokichakata. Kimsingi watafiti wamebaini makundi makuu matatu ya watu kuhusiana na jinsi miili inavyochakata chakula.

Kundi la kwanza ni la wachakataji wa protini. Hawa miili yao inakubaliana zaidi na vyakula vya protini. Kwa watu wa kundi hili vyakula vya wanga na hususan vile vilivyochakatwa na kuchujwa kwa kiwango kikubwa (highly processed and refined), ni sumu baridi ambayo itawapelekea kuugua maradhi mengi ya kimfumo.

Kundi la pili ni la wachakataji wa wanga. Hawa miili yao inakubaliana zaidi na vyakula vya wanga. Kwa watu wa kundi hili la vyakula vya protini, hususan vile vilivyochakatwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kuwa na muda mrefu wa matumizi, ni sumu baridi ambayo itasababisha kuugua maradhi mengi ya kimfumo.

Kundi la tatu ni la wachakataji wa vyakula vya protini na wanga kwa viwango sawa. Kundi hili kidogo lina bahati, kwa maana, halidhuriwi kwa wepesi na vyakula vilivyoko katika yale makundi mawili ya mwanzo.

Moja ya magonjwa yanayosababishwa na mkanganyiko huu katika kula ni ugonjwa wa kisukari. Mchakataji wa protini anapokula chakula cha wanga, kasi ya kuchakata wanga huo ni kubwa mno ikilinganishwa na mlaji mwenzake ambaye ni mchakataji wa wanga.

Kasi hiyo husababisha kiwango cha sukari kinachoingia katika mzunguko wa damu ndani ya muda mfupi kuwa kikubwa sana. Kutokana na hali hii kongosho hulazimika kufanya kazi ya ziada kuzalisha kiwango kikubwa cha kichocheo kinachojulikana kama insulini ili kuondoa sukari kwenye damu na kuipeleka kwenye seli ili itumike kutengenezea nishati.

Hali hii ikijirudiarudia, kongosho huchoka na kuanza kufanya kazi chini ya kiwango au wakati mwingine vipokezi vya sukari katika seli (receptors) hushindwa kuendana na kasi ya kuletewa sukari kwa ajili ya matumizi ya seli hivyo huishia kuikataa sukari hiyo.

Hali hii kitaalamu hujulikana kama insulin resistance, au pingamizi dhidi ya insulini kwa tafsiri isiyo rasmi. Kuna baadhi ya nyakati, vyote hutokea kwa wakati mmoja, yaani kongosho linafanya kazi chini ya kiwango, na pia mgonjwa anakabiliwa na pingamizi dhidi ya insulini.

Hivi karibuni imebainika kuwa moja ya sababu kubwa sana zinazosababisha vipokezi vya seli kushindwa kupokea sukari inayoletwa ni kitu kinachoitwa mfuro (inflammation). Mfuro ni uvimbe kama lengelenge hivi. Mfano wa mfuro ni pale unapojikwaa au kujigonga usoni na mwili ukaumuka na kutengeneza nundu.

Vichocheo vya kusababisha mfuro kwenye seli viko vingi lakini baadhi ya hivi ni vyakula tunavyokula kila siku. Vyakula hivi ni pamoja na sukari na wanga uiliochakatwa kwa kiwango kikubwa.

Athari za ugonjwa

Kisukarini ni ugonjwa ambao unasababisha mololongo wa matatizo mengine ya kiafya mwilini. Matatizo haya ni pamoja na uharibifu wa macho, unaotambulishwa na magonjwa kama glaucoma ambao husababisha uharibifu wa neva za jicho.

Matatizo mengine ni ugonjwa ujulikanao cataracts ambao unatokana na ukungu kwenye lenzi ya jicho na retinopathy unaosababisha uharibifu katika retina ya jicho.

Matatizo mengine ni ya miguu yanayotambulishwa na magonjwa kama neurapathy ambayo ni maumivu yatokanayo na uharibifu wa mishipa ya fahamu, vidonda sugu vya tumbo na gangrene ambao ni mkusanyiko wa tishu zilizokufa kutokana na kutofikiwa na mzunguko wa damu.

Matatizo mengine ni yale ya magonjwa ya ngozi na magonjwa ya moyo.

Mpango mzuri wa kuudhibiti ugonjwa wa kisukari ni kuufuatilia kwa makini. Hii ina maana kuwa ni muhimu kufanya kipimo kila siku, ikiwezekana hata mara mbili au tatu kwa siku. Kutokana na hali hii gharama za kuufuatilia ugonjwa huu ni kubwa na huathiri kwa kiasi kikubwa hali ya kiuchumi ya mgonjwa.

Kwa mfano tu, hivi sasa katika zahanati na vituo vingi vya afya, gharama za kupima kisukari kwa mara moja ni kati ya Sh2,000 na Sh2,500.00. Unapomwambia mtu apime mara tatu kwa siku maana yake atumie kati ya Sh6,000 na Sh7,500.00 kila siku.

Ugonjwa wa kisukari kwa sasa kinaonekana kunyemelea hadhi ya kuwa ni janga la kijamii. Katika pande zote za dunia kisukari kinaongezeka badala ya kupungua. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), dunia inatarajiwa kuwa na wagonjwa wa kisukari milioni 366 mwaka 2030 kutoka wagonjwa milioni 171 waliokuwepo mwaka 2000.

Mwaka 2000 Tanzania ilikuwa na wagonjwa 201,600 na mwaka 2030 inatarajiwa kuongezeka maradufu na kufikia 605,000. Hili ni sawa na ongezeko la asilimia 66.7.

Hata hivyo janga la kisukari linaoonekana kuzikumba zaidi zile nchi ambazo raia wao wanapendelea mno vyakula vya wanga katika mitindo tofauti.

Vyakula hivyo ni soda, pasta, doughnut, keki, mikate, lambalamba, nakadhalika. Nchi kama Italy uwiano kati ya Wataliano wanaoumwa kisukari na wale ambao hawaumwi ni mtu mmoja kati ya 14. Inawezekana sababu kubwa ikawa ni ulaji wa piza, pasta na spaghetti. Hivi ni vyakula vinavyotengenezwa kwa ngano na Wataliano wanapenda kuvila kwa wingi.

Marekani uwiano wao ni mtu mmoja kwa kila watu 17. Hii nayo ni jamii ambayo inatumia soda, doughnut, chips, pizza, na vyakula vingine vya wanga vilivyochakatwa kwa kiwango cha juu. India uwiano wao ni mtu mmoja kati ya 39. Hawa nao ni mabingwa wa vitu vitamu. Wahindi wanapenda tamutamu za kila aina na sifa kuu ya vitu hivyo ni wingi wa sukari, ngano, mafuta na rangi.

Tanzania ina uwiano wa mtu mmoja kati ya 238. Huu ni uwiano mzuri sana ukilinganisha na nchi tulizotangulia kuzitaja. Sababu ya uwiano huu mzuri ni nini? Kimsingi sehemu kubwa ya Watanzania ni wala wanga zaidi kutokana na hali zao za kiuchumi?

Nadhani sababu kubwa ni ukweli kwamba Watanzania wengi ni wakaazi wa vijijini na kimsingi pamoja na kwamba sehemu kuwa ya chakula chao ni wanga, lakini kutokana na sababu za kiuchumi, wanalazimika kuula wanga huo katika mfumo ambao haujachakatwa.

Apple to launch Apple TV on September

September is set to be full of surprises from Apple...New Iphone,new ipad and now,rumor of an Apple TV can not be ignored. No,am not talking about an actual TV set but rather the baby below...

 It is rumored that Apple will launch this baby on September,bringing all the fun at home..whereby movies,music,games etc are all a click away


From their website,i got this description..."Apple TV gives you access to tons of great HD content in a tiny package. Enjoy blockbuster movies, TV shows, live sports and news, your music, photos, and more — right on your high-definition TV. You can even play content from your iOS devices or Mac on your TV using AirPlay. Best of all, Apple TV is just $69."..
I can't imagine where tech will take us next....

Are you excited about this new Apple product?

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...