Mtu anayeongoza mazungumzo ya
kuachiliwa huru kwa wahubiri saba wa kiislamu kutoka Tanzania waliotekwa
nyara wiki iliopita ameiambia BBC kwamba makubaliano ya kuwaachilia
huru huenda yakaafikiwa hivi karibuni.
Sheikh Suleiman Mohammed
amesema kuwa kundi la watu wanaofanya mazungumzo hayo limewasiliana na
watekaji nyara hao na kwamba viongozi hao wa dini hawajateswa.''Wametaka kupewa fedha ili kuwahudumia mateka hao iwapo fedha za fidia hazitalipwa'',aliambia BBCswahili.
Ameongezea kuwa maimamu hao sio waliokuwa wakilengwa na washambuliaji hao na kwamba walikuwa katika mahala pabaya katika wakati usiofaa.
No comments:
Post a Comment