10 August, 2015

Weusi 2 wapigwa risasi Ferguson,Marekani


Mtu mmoja amejeruhiwa vibaya huko Ferguson, Missouri, huko Marekani baada ya kisa cha ufyatulianaji risasi uliotokea katika dakika za mwisho mwisho za maandamano ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuuawa kwa mvulana mweusi Michael Brown na polisi mwaka uliopita.
Kisa hicho cha mauaji kilisababisha mtafaruk baina ya watu wa jamii ya wamarekani weusi na polisi.
Barubaru huyo tayari amefanyiwa upasuaji na anasemekana hali yake ya afya imedhibitiwa kwa mujibu wa polisi.
Polisi wanasema kuwa walikuwa wakimsaka barubaru huyo kwa kipindi kirefu baada ya kupokea habari kuwa alikuwa amejihami kwa bunduki iliyoibwa.
Jina la mhasiriwa huyo halijajulikana kufikia sasa.
Mkuu wa polisi katika jimbo hilo la Ferguson Jon Belmar amesema kuwa tayari maafisa 4 wa polisi wamehssimamishwa kazi ilikufanikisha uchunguzi wa kina kuhusu kisa hicho.
Picha kutoka eneo la tukio zinaonesha mtu mweusi anayetokwa na damu akiwa amelala sakafuni.
Awali,mamia ya watu walisimama kimya kwa muda wa dakika nne na nusu kwa pamoja mjini Ferguson ,Missouri katika sehemu ile ile ambayo kijana asiye na hatia Michael Brown aliuwawa na polisi mmoja wa kizungu mwaka mmoja uliopita.
Ishara hiyo inaashiria muda ambao mwili wake ulilala katikati ya barabara bila kupata msaada wowote.
Njiwa wawili walipeperushwa hewani na watu waliandamana kimya kimya ili kutoa heshima kwa Michael Brown na wengine ambao walikufa katika mikono ya polisi.
Mauaji hayo yalileta mjadala dhidi ya ubaguzi wa polisi nchini Marekani na ulimwenguni.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...