Twiga Stars iko kambini visiwani
Zanzibar kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games)
zitakazofanyika nchini Congo- Brazzavile kuanzia Septemba 04–19 mwaka
huu.
Kocha Mkuu wa Twiga Stars,
Rogasian Kaijage ameendelea kukinoa kikosi chake cha wachezaji 25
waliopo kambini visiwani Zanzibar kujiandaa na michuano hiyo ya Afrika.
Twiga Stars itakua kambini kwa
kipindi cha mwezi mmoja, kujiandaa na fainali hizo za michezo ya Afrika,
ambapo imepangwa kundi A pamoja na wenyeji Congo-Brazzavile, Ivory
Coast na Nigeria.
No comments:
Post a Comment