Daktari
wa Chelse Eva Carneiro amewashukuru mashabiki waliomtia moyo baada ya
kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho kuishambulia timu ya matabibu akisema
kwamba ni ‘wajinga’.
Katika
sare ya goli 2-2 dhidi ya Swansea kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi kuu
ya England, Mourinho alichukizwa na kitendo cha Carneiro kuingia
uwanjani kumtibu Eden Hazard na kutumia muda mrefu ilihali dakika zikiwa
zimesalia chache.
Wakati huo Chelsea walilazimika kubaki 9 uwanjani na Swansea wakapata fursa ya kulisakama lango la Chelsea.
Mourinho alisema daktari huyo hakuelewa mchezo.
Carneiro amesema: “Napenda kuwashukuru watu wote walionipa moyo. Kiukweli nimepata faraja sana”.
No comments:
Post a Comment