Takriban watu 10 wameuawa na wengine
20 kujeruhiwa katika mkanyagano uliofanyika katika hekalu moja katika
jimbo la mashariki la Jharkhand nchini India .
Mahujaji wamekuwa wakiadhimisha sherehe ya kidini ya Hindu katika mji wa Deoghar.Kisa hicho kilitokea wakati mahujaji walipokuwa wakiingia ndani ya ukumbi huo.
Mikanyagano mibaya hutokea mara kwa mara nchini India wakati wanapoadhimisha sherehe za kidini ambazo huvutia makundi makubwa ya watu bila ya kutilia maanani usalama.
Mkanyagano huo katika hekalu la Baidyanath Jyotilinga ulianza baada ya mahujaji kuelekea eneo takatifu mda mfupi baada ya milango kufunguliwa siku ya jumatatu.
No comments:
Post a Comment