26 August, 2016

Wizkid kuungana na Davido Sony Music Worldwide

Mwanamuziki maarufu Nigeria na Africa kwa ujumla Wizkid yuko mbioni kutangazwa msanii mpya wa Sony Music Worldwide, kwa mujibu wa kituo cha runinga cha Soundcity.Kituo hicho kimeripoti kuwa muimbaji huyo ataungana na Davido kwenye roaster ya label hiyo kubwa.
“Dili la Wizkid na Sony limekamilika. Habari itatoka hivi karibuni. Meneja wake Sunday Are ametuelezea kuwa hili litazungumzwa hivi karibuni,” kilisema chanzo.
Umaarufu wa Wizkid umeongezeka maradafu mwaka huu baada ya kushirikishwa na Drake kwenye wimbo One Dance ulioshika namba moja kwenye chati za Billboard Hot 100.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...