26 August, 2016

Mr. Nice apata shavu la kupiga show 47, ataja wasanii wakubwa waliomuomba kolabo

nic  Mwanamuziki mkongwe katika Burudani ya muziki na mwanzilisha wa ‘Takeu style’, Lukas Mkenda almaarufu kama Mr. Nice, amepata shavu kutoka katika kampuni moja ya Nigeria ambayo imempatia mkali huyo shows 47 ambazo atazifanya katika County mbali mbali huko nchini Kenya ambapo ndipo alipo kwa sasa akiendesha shughuli zake za Muziki. 
“Niko huku Kenya,kuna kampuni ya Nigeria imenipa dili la kufanya tour kwenye county zote za Kenya, ziko 47″ Mr. Nice aliiambia Radion one.

Pia Mr.Nice amesema ana project mpya na Jaguar na Wyre ambazo zitatoke hivi karibuni,
“Pia nina project na wasanii wengine wa Kenya ambao wameniomba nifanye nao kazi,tuko na project na Jaguar na nyingine na Wyre kwa hiyo soon mambo yatakuwa mazuri
Kila la Kheri Bro!

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...