John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu
chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika
kuwa hela anayoacha nyumbani haitoshi, au akichelewa kurudi mke wake
humsingizia John kuwa ana wanawake wengine huko nje ndio kisa cha
kuchelewa kurudi nyumbani, hata John akitoka na marafiki pia ni tatizo
kubwa.
John anasema muda mwingine anatamani hata
aanze kumpiga mke wake kwakuwa mambo anayolalamika au anayoyasema si ya
kweli. Mke wake anashindwa kuuliza maswali kwanza bali anaanza
kulalamika na kumsingizia vitu vingi.
John anasema alianza pole pole kufanya
vitu mke wake alivyokua akimsingizia kwani alianza kuchelewa kurudi
nyumbani ili asikutane na mke wake, na baadaye akapata mwanamke mwingine
na kuanza kunywa pombe.
John anasema matendo aliyoyafanya yalifanya ndoa yake izidi kuharibika na mke wake ndio alizidisha gubu.
Hili jambo hutokea sana kati ya wanandoa
na sio mwanamke tu anayekua hivo, hata wanaume nao, Gubu, malamiko
lazima itatokea katika mahusiano, inategemea tu ni jinsi gani mnaweza
kuihandle na kuzuia matatizo makubwa zaidi.
JINSI YA KUISHI NA MWANAUME AU MKE MWENYE GUBU sio rahisi lakina inawezekana,
- Kwanza kabisa unatakiwa uwe msikivu, hili tatizo linaanza pale mwanaume/mke akiwa na malalamiko lakini mwenzako hawi msikivu. Hii itapelekea mwenzako kuona kuwa huna time naye na hujali vitu anavyokwambia, na hivyo huyo mtu ataanza kulalamika na kufiria sababu zingine kabisa za kwanini humsikilizi kama vile kuwa na mpenzi mwingine nje ya mahusiano yenu.
- Jaribu kuwa muelewa, kama mambo yameshakuwa mabaya kati yenu jaribu kuwa muelewa, acha kujibu malalamiko ya mwenzako kwa kufoka au kwa vurugu. Jaribu kufikiria ni kitu gani kinachomfanya mwenzako awe hivo na kuongea nae.
- Kwa wanawake mpunguze dharau, hasira na malalamiko yasiyo na mbele wala nyuma kwa waume zenu, na msizue matatizo yalipita. Focus katika tatizo lililopo ili muweze kulisolve.
- Kwa wanaume, mnatakiwa kuwasikiliza wake zenu, sikiliza malalamiko waliyokuwa nayo, myaongelee na kuyasolve matatizo.
Wanandoa wakishindwa kutatua matatizo kama
haya, chuki inakua kati yao na ndoa inazidi kuwa chungu, na matumaini
ya kusolve matatizo kati yao yanakuwa hamna tena, na hii inaweza kuwa
mwisho wa mahusiano yao.
Wewe je, unaishi na mwanaume au mwanamke
mwenye gubu? Unawezaje kuishi nae, au unafanya nini ili kuweza kumhandle
na kuepuka matatizo kati yenu?
Mie naishi nae, lakini nimezingatia sana point hii ya kumsikiliza anachosema na kufanya kile ameniagiza, ni mwaka mmoja sasa nipo nae.
ReplyDelete