Bomu lililotegwa ndani ya gari
limelipuka nje ya mgahawa mmoja uliopo katika ufukwe wa bahari katika
mji mkuu wa Somalia Mogadishu,kulingana na maafisa wa polisi.
Walioshuhudia
wamemwelezea mwandishi wa BBC Ibrahim Aden kwamba gari hilo lililojaa
vilipuzi liligonga mgahawa huo maarufu wa Lido Beach kabla ya watu
watano kujitokeza na kuanza kufyatua risasi.Haijulikani iwapo kumekuwa na majeruhi.
Hakuna kundi lililokiri kutekeleza shambulizi hilo,lakini kundi la Alshabaab ndilo linaloshukiwa kwa kutekeleza mashambulizi mengine kama hayo hapo awali.
Mgahawa wa Lido Beach uliopo pembezoni mwa Mogadishu,huwavutia maelfu ya vijana wa Somalia wanaojifurahisha.
Migahawa kadhaa imefunguliwa katika ufukwe huo katika miaka ya hivi karibuni.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Meja Abdiqadir Ali amekiambia chombo cha habari cha reuters kwamba shambulio hilo lilitokea katika lango la mgahawa huo.
Amesema kuwa uchunguzi unaendelea.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment