22 January, 2016

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI MKOANI ARUSHA APOKELEWA NA UMATI WA WANANCHI KIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro leo huku akiongozana na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda tayari kwa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya wa jeshi la Wananchi waliohitimu vyema mafunzo yao katika chuo cha Jeshi Monduli Mkoani Arusha itakayofanyika Januari 23 /2016. PICHA NA IKULU 
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akishiriki kupiga ngoma za utamaduni wakati alipowasili kwenye uwa nja wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waliofika kwenye uwanja wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kumlaki uwanjani hapo.Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro. Baadhi ya wananchi wakimpungia mikono Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA mkoani Klimajaro.Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waliofika kumlaki uwanja wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro.Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ukiondoka kwenye uwanja wa ndege wa KIA kuelekea Arusha mjini.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...