22 January, 2016

Yanga yaizamisha Majimaji

Yanga 4
Amis Tambwe ameibuka shujaa kwenye mchezo wa Yanga vs Majimaji baada ya kutupia kambani goli tatu (hat-trick) wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa bao 5-0 na kupaa tena hadi kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Yanga walianza kupata bao lao la kwanza kupitia kwa Thabani Kamusoko ambaye alipachika bao hilo dakika ya nne kipindi cha kwanza kwa kutumia makosa yaliyofanywa na golikipa wa Majimaji FC David Burhani aliyesogea mbele na kuliacha lango lake wazi.
Yanga 1
Bao hilo lilidumu hadi dakika zote za kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga wakiwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Majimaji.
Donald Ngoma alipachika bao la pili dakika ya 50 kipindi cha pili na kuiweka Yanga mbele kwa bao mbili mwanzoni mwa kipindi cha pili.
Yanga
Gharika ya magoli ilianza baada ya Majimaji kuruhusu bao la pili, kwani Amis Tambwe ndiyo ukawa muda wake wa kutafuta (hat-trick) nyingne kwenye ligi ya msimu huu. Dakika ya 60 Tambwe alizama wavuni kuiandikia timu yake bao la tatu huku likiwa ni bao lake la kwanza kwenye mchezo wa leo.
Tambwe alipachika bao jingine la pili akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Deus Kaseke ambaye alimuwekea krosi Tambwe naye akaitupia kwenye nyavu. Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Burundi alikamilisha hat-trick yake dakika ya 84 baada kupiga goli safi kufuatia beki wa Majimaji kujiangusha kwenye eneo lake la hatari na kutoa mwanya kwa Tambwe kufunga goli kwa urahisi.
Yanga 2
Mchezo wa jana ulikuwa ni wa pili kwa Kally Ongala tangu akichukue kikosi cha Majimaji akiwa kama kocha mkuu wa timu hiyo na kujikuta akiambulia kichapo cha nguvu kutoka kwa Yanga.
Mchezo wa jana ni wa pili kwa Majimaji kupoteza kwa idadi kubwa ya Magoli wakati mchezo wao wa kwanza kupoteza kwa kipigo kikubwa ulikuwa ni dhidi ya Simba walipokubali kulala kwa bao sita.
Yanga 3
Kikosi cha Yanga: Deogratias Munishim Kelvin Yondani, Juma Abdul/Said Juma ‘Makapu’, Oscar Jushua, Vicent Bossou, Salum Telela, Simon Msuva/issoufou Boubcar, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma/Paul Nonga, Amis Tambwe na Deusi Kaseke.
Kikosi cha Majimaji: david Burhani, Alex Kondo, Bahati Yusuph, Mpoki Mwakinyuke, Sadiq Gwaza, Lulanga Mapunda/Kened Kipepe, Peter Mapunda/Hassan Hamisi, Paul Mahona/Gogfrey Taita, Marcel Bonaventura, Sixmund Mwakasega na Frank Sekule.
Matokeo ya mechi nyingine zilizopigwa jana kwenye viwanja tofauti na uwanja wa taifa ni kama ifuatavyo:
Mwadui FC 2-1 Kagera Sugar
Mtibwa Sugar 0-0 African Sports

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...