23 January, 2016
Je PEP GUADIOLA atakwenda MANCHESTER UNITED ?
Manchester United wamekanusha kwamba walikutana na boss wa Bayern Munich Pep Guardiola kuhusu uwezekano wa kuchukua mikoba ya bosi sasa Louis van Gaal, baada ya soka Ufaransa kusema kuwa mkutano ulifanyika jana mjini Paris, lakini United wamesisitiza kuwa hadithi hizo sio za kweli.
Guardiola, 45, ataondoka Bayern Munich mwisho wa msimu huu huku akisema kuwa anataka kufundisha soka nchini England.
Manchester City ndio wanaopewa kipaumbele kumnasa Mhispania huyo, lakini Chelsea na Manchester United wao pia wamekuwa wakihusishwa pamoja na kutaka kupata huduma ya bosi huyo.
Bayern Munich wapo katika kambi ya mafunzo mjini Doha katika mapumziko ya baridi huku ligi kuu nchini Ujerumani ikitarajiwa kurudi tena wikend hii ambapo Bayern Munich watacheza mchezo wao dhidi ya Hamburg siku ya Ijumaa.
Guardiola, ambaye mkataba wake na Bayern unafikia tamati katika majira ya joto, hapo awali alisema ana nia ya kufundisha soka nchini England, hali iliyosababisha presha kubwa kwa makocha wa timu za City na United ambao timu zao hazina muelekeo mzuri sana katika ligi.
Tayari Pep Guadiola amewaomba radhi makocha nchini England kama kauli zake za kutamka kutaka kufundisha soka nchini England zimesababisha presha miongoni mwao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment