07 June, 2016

Mambo ambayo hupaswi kufanya pindi unapo fika mika 24.

Street theater 
 Katika maisha ya mwanadamu, mambo huenda yakibadilika kulingana na Umri na muda husika hivyo kuna mambo ambayo mtu akifika umri na muda fulani hupaswa kuyafanya na mengine hapaswi kufanya tena.

 Kama inavyo julikana kwamba umri wa miaka 24 ni umri ambao kijana ana hesabika kwamba kakamilika katika idara zote(Kielimu,kiakili na fikra,) wengi walio vijanakatika kundi hili ni wale ambao wamemaliza(Wamehitimu) masomo yao katika Vyuo mbali mbali, hivyo wanakua teyari kuanza maisha wakiwa peke yao. Wengine hapa ndio muda wa kuanzsa kufanya yale walio kuwa wakitaman kufanya pindi wakiwa masomoni mfano Biashara na vitu kama hivyo na wengine huwa bado katika njia panda(hawajui bado nini chakufanya kwa wakati huo).

Kabla sijaendelea tafadhali pitia hizi zifuatazo kwanza:-

1.Acha kuogopa na thubutu kufanya

2.Viashiria 6 ni kwa nini unatakiwa kubadili maisha yako leo

3. Kanuni 9 za mafanikio kutoka kwa Steve Jobes

4. Tuzungumzse yanayo tusibu na kupata suluhisho

Baada ya kupitia hapo juu basi tuendelee na Mada yetu ya leo na haya yafuatayo ndiyo mambo ambayo hupaswi kufanya tena baada ya kufika umri wa mika 24...

 Acha/punguza kuvaa nguo za Bei rahisi.

Wakati ukiwa teeneger ulikua unavaa nguo za bei chee na kubadili kila wakati, lakini kwa sasa umeingia ukubwani na una unategemea/unafanya kazi ya maana , hivyo unapaswa kuwekeza katika mavazi ya maana na stlyes tofauti tofauti za maana.

Acha kuwa na mahusiano(mapenzi) na mtu ambaye haendani na wewe.

Nafahamu swala la mapenzi linatesa sana vijana tulio wengi na linapo kuja
swala la kuwa na mahusiano na mtu ambaye ni wa aina yako hapo ndipo Ungumu huonekana kweli kweli, lakini yakupasa kuchukua mda mrefu kuchanganua "who is suitable for you" na kwa wakati gani. Usipoteze muda wako kuwekeza kwa mtu unaye mjua ndani nje kuwa haendani na wewe ila tamaa tuu ndio zinakufanya kuwa nae.

Punguza kujali wanacho kisema wengine.

Ni hali ya kawaida kwa mwanadamu kuhofia kile wanacho kisema wanadamu wengine, lakini mengine huwa ni mambo ya kukandamizana tuu. Hivyo punguza ama acha kusikiliza wanacho kisema maana itafika kipindi utakata tamaa na kubadili malengo yako kisa tuu maneno ya wanadamu wa duni hii ya leo na hata inaweza kufika pahala ukatamini kujiua.

Acha kuwalaumu wazazi.

Nafahamu kwamba vijana tulio wengi tumetokea kwenye familia za kimasikini na maisha yetu ya leo kwa namna moja ama nyingine yamesabashwa na familia tulizo kulia. Kuna wakati maumivu ya umasikini hutuchoma mithili ya moto wa gas na kufika pahala tunasema "Laiti wazazi wangu wangekuwa......." au "Bora ningezaliwa Mbwa/paka ulaya" no no noooo punguza kusema hivyo na kumbuka kwamba umekwisha kuwa mtu mzima una akili, nguvu na Chance ya kutoboa. Hakuna mzazi aliye kamilika jamani.

Acha kuwa tena na matumaini ya ndoto zako bali fanya kweli.

Siyo vibaya kwa kijana kuzidi kuwa na matumaini juu ya ndoto zake lakini inapaswa ifikapo muda fulani, basi tumaini hilo litime na kuonekana katika maisha(Hiyo ndio maana ya tumaini). Jaribu kufanya kile ulicho wahi kukitumainia na kukiota enzi za udogo wako maana huu ndio wakati wa kufanya kweli.

Punguza kutumia muda mwingi kwenye Internet.

Jambo hili ni ngumu kwa kijana wa leo. Hili jambo limekuwa tegemezi kiasi kwamba mtu hawezi kukaa bila mtandao. Watu wanatafuta mambo mitandaoni, wanajinga na marafiki na mambo mengi kibao. Lakini unapaswa kutenga muda na kuwa na mipaka katika hili maana jambo hili ni moja kati ya mambo yanayo poteza muda wa mwanadamu kuliko kitu chochote.

Hitimisho.
Yapo mambo mengi ambayo wewe kama kijana mwenye umri huu hupaswi kufanya maana utu uzima umekufika teyari huvyo basi, yale yote uliyo yafanya tangu ukiwa shuleni unapaswa kuyatupilia mbali na Kufanya mambo kiutu uzima zaidi.

"NIWATAKIE WAISLAMU WOTE RAMADAN KAREEM"

 

 

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...