Mtu mmoja alipata kusema "Hasara roho, pesa makaratasi" na mimi nasema ni kweli kabisa.
Je una Amani ya moyo mwako? Je uhuru ulio nao unautumiaje? Je ukitazama ndani ya Fikra zako unaona Mafanikio yeyote? Je una imani juu ya ndoto zako? Je una mpango wowote juu ya Kuthubutu kuishi ndani ya Ndoto zako?.....
Leo nimepanda hapa MTOKAMBALI nikiuliza maswali hayo nikiwa na maana ya kwamba maswali hayo Yamekuwa chachu ya Mafanikio ya mtu yeyote hapa Ulimwenguni,,, Huwezi niambia ya kwamba utaweza kufanikiwa katika mambo yako angali Huna Amani Moyoni mwako wala kufanikiwa wakati umeshindwa kuutumia vyema Uhuru ulio nao ama Kufanikiwa angali hujawahi kuthubutu kufanya chochote juu ya ndoto zako...
Licha ya kuishi katika nchi yenye Uhuru lakini bado kuna vijana wenzangu hawana UHURU katika maisha yao. Wamekuwa wakiishi kama watumwa, wamekuwa wakipoteza hata matumaini yakuishi.. Hii yote inasababishwa na KIFUNGO CHA FIKRA.
Acha nikuambie rafiki yangu,
Hakuna jambo la muhimu na lenye nguvu katika maisha ya mwanadamu awaye yeyote hapa ulimwenguni litakalo weza kuishinda nguvu ya Fikra.(Weka kumbu-kumbu juu ya mstari huu tafadhali).
Kile ambacho unafikiri kwa Muda mrefu ndicho kitakachotokea katika maisha yako. Fikra zako zina nguvu ya uumbaji.. na zaidi ya yote fikra zako ndizo zitakazo kupatia Uhuru wa kweli katika maisha yako na mafanikio tele utayaona. Ila pale unapokuwa mtumwa wa fikra zako, hakika utatamani kuiona Ardhi inapasuka kisha Uingie ndani yake na kupotea katika ulimwengu huuu wenye dhiki tele.
Leo nitakupatia njia ambazo zitakufanya uondokane na Utumwa wa fikra zako na kisha kupata uhuru wa Fikra zako na kufanikiwa kuishi katika baadhi ya ndoto zako. Tambua yakwamba njia hizi nitakazo kupatia, ni njia ambazo nilizitumia mimi kipindi nikiwa Utumwani na hadi Leo nathubutu kusema "NIKO HURU".
Je uko teyari? lets move-on...
1. Jiamini unaweza
Katika maisha ya mwanadamu ni lazima kila mmoja ajiamini kwamba anaweza. Mwana harakati mmoja aliwahi kusema "Uoga wako ndio umasikini wako". Njia ya kwanza ya kutoka katika kifungo cha fikra zako ni kuamini kwamba unaweza kuleta mabadiliko yeyote katika maisha yako licha ya hali uliyo nayo. Amini kwamba utaweza kuboresha maisha yako yakawa bora zaidi kama tuu utaongeza bidii katika hilo.
2.Ondoa Mawazo hasi katika maisha yako.
Moja ya maadui wakubwa wa Uhuru wa fikra za mwanadamu na Maisha kwa ujumla ni Fikra hasi(potofu). Fikra hasi huwa na hulka ya kukua kidogo kidogo katika maisha ya mwanadamu awaye yote yule na mwishoni huleta maafa makubwa mno na majuto yale ya mjukuu. Ili kuepuka hali hii unapaswa kuchukulia mambo kwa upande wa chanya zaidi kuliko upande wa hasi... hii itakusaidia sana katika kufikiri kwenda mbele ya mafanikio yako. Fikra hasi hupoteza matumaini siku zote hivyo yakubidi kuziepuka.
3.Epuka kuchukulia mambo kwa ujumla
Kuna vijana wengi huchukulia mambo kirahisi kama yalivyo na mwisho wa siku wanajikuta katika hali ngumu mno katika maisha yao. Embu jaribu kuchambua jambo moja moja kwa kina kisha ainisha ni lipi jema na ni lipi baya katika huo ujumla ulio nayo. Kumbuka unapokuwa ukichukulia mambo kwa ujumla, hutopata changamoto yeyote ile ambayo itakufanya Kufikiri kwa kina.
4.Thubutu kufanya.
Njia nyingine ya kutoka katika utumwa na kuupata uhuru wako ni kuthubutu kufanya kile ulicho nacho katika fikra zako juu ya maendeleo yako. Natambua kila mmoja wetu hapa ana ndoto fulani kubwa katika maisha yake na kama( huna ndoto yeyote katika maisha yako jua una hali mbaya kupindukia..). Je uliwahi kujaribu kuifika hata nusu ya ndoto zako? kama jibu ni ndio basi endelea na safari maana bado kidogo utafika mpendwa na kama bado hujathubutu basi kwa nzia sasa thubutu.
5.Acha kufanya mambo mengi kwa mawazo yako.
Mwanadamu hajakamilika siku zote na kila mwanadamu ana mapungufu yake , hivyo mapungufu yako wenda ikawa mwenzako anaweza kuyatua na wewe pia unaweza kuyatatua, hivyo utaona ni kwa namna gani utakapo kuwa ukishirikiana na wenzako katika kutimiza mambo yako utafanikiwa zaidi kuliko kufanya peke yako..
6.Jali muda wako.
Nafahamu kwamba kwa asilimia kubwa mno vijana wengi wamekuwa wakipoteza muda wao katika mambo yasiyo na msingi na mwisho wa siku wanajikuta hawajafanya mambo yaliyo wapasa kufanya kwa wakati ule na kuanza kujuta ni kwa nini..... Embu kabla ya kupata majuto, jaribu kufanya mambo katika muda husika bila hata kupoteza sekunde moja katika Muda wako. "Majuto ni mjukuu"
Kwa kusema hayo, nammba nikwamie hapo na ni matumaini yangu kwamba nimekupatia kile unachokihitaji. Nimejfunza mengi mno katika maisha haya licha ya Umri wangu mdogo nilio nao. Likini kwa kuwa naamini katika ndoto zangu, sioni kama naumia bali nayaona maisha yangu katika Ulimwengu wa mafanikio.
Je umependa somo langu? Tafadhali niachie maoni yako hapo chini.
NINEPENDA PIA UPITIE NA HIZI:-
>>>> Viashiria 6 ni kwa nini unatakiwa kubadili Maisha yako Leo
>>>> Furaha ya kweli inaletwa na wewe mwenyewe.
>>>> Amani ya Moyoni mwako ndio Kunawiri kwa Uso wako.
No comments:
Post a Comment