06 June, 2016

Page za Mark Zuckerberg zimedukuliwa(Hacked)


Hapa ndipo pale ninapo amini kweli mganga hajigangi. Mark Zuckerberg mwanzilishi wa Facebook hapo jana aliiionja joto ya jiwe baada ya Kurasa zake za Mtandao wa LinkedIn, Twitter pamoja na Pinterest kudukuliwa(Hacked) kwa muda wa siku ya juma pili.

Kundi moja la Hackers linalo julikana kwa jina la Ourmine limedai kuzidakua akaunt hizo za Mark. Kundi hilo liliandika ujumbe katika ukurasa wao wa twitter likimtaka Mark awafuate(awasiliane nao). 
Hey @finkd we got access to your Twitter & Instagram& Pinterest, we are just testing your security, please dm us"  

Akount hizo zilirudishwa tena mikononi mwa Mark baada ya kazi nzito ilofanywa na wataalamu wa usalama wa mitandao kumudu kuzidhibiti saa chache baadaye. Ifahamike kwamba tangu mwaka 2012 Mark haja posti kitu chochote katika kurasa hizo. 

Kutokana na mfumo imara wa mtandao wa Instagram, uliwafanya Hackers hao kushindwa kudakua ukurasa wa Mark.Wandani wa maswala ya usalama wa mitandao ya Intaneti wanadai kuwa huenda udukuzi wa mwaka wa 2012 wa ukurasa wake wa LinkedIn ndio uliochangia tukio hilo la jana.

MY TAKE! Kuweni makini na mitandao hii ya kijamii maana usalama wa mitandao hii siyo wa kuamini moja kwa moja.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...