“Kuzaliwa Masikini Sio Kosa Lako, ila Kufa Masikini ni Kosa Lako Kubwa Sana”Msingi wa kufanikiwa ni kuthubutu kufanya jambo fulani kwa mfano kufungua miradi, kufanya biashara, kusoma kwa bidii na mambo mengine kibao.
Ngoja nikuulize tena, maana najua utakua ushaulizwa hili swali mara
nying, Hivii unatamani kuishi au uwe kama nani ? wengi wetu mtasema
natamani kuishi maisha mazuri na bora.
Hii iko hivi unapozungumza na watu wote duniani kila mtu atakwambia kuwa
anataka kuwa na maisha mazuri ,huenda na ni vigumu kwa mtu wa kawaida
kusema anataka maisha yake yawe ya shida kila siku. Huyo atakua ana
lake.Wewe una stashahada una shahada na elimu nyingine nyingi, sijui
umeahudhulia workshop kama ishirini, ila ndugu yangu bado utaendelea
kuchapwa bakora na maisha kama hautakuwa makini na kuthubutu kufanya
mambo unayotamani kufanya.
Kusoma sana ama kidogo kuwa na marafiki
waliofanikiwa ama wasiofanikiwa,kwenda nje ya nchi ama au kuzaliwa
katika familia masikini au tajiri bado sio tiketi ya kukufanya uwe na
maisha bora .
Kuna watu kwa mfano unaweza kuona anakata tamaa eti kisa amezaliwa
katika familia maskini kitu ambacho sio sahihi.Bill Gates alisema
“Kuzaliwa Masikini Sio Kosa Lako, ila Kufa Masikini ni Kosa Lako Kubwa
Sana”
Yaani anamaanisha duniani kuna fursa nyingi sana ambazo unaweza kuzitumia na kuwa na maisha unayoyataka.
Kuwa na maisha bora ni kufanya kazi kwa bidii na kwa malengo zaidi
usiishi tuu ilimradi siku zinaenda mbele. Kwa chochote unachokifanya
kifanye kwa kutafakari na kuangalia faida na hasara yake.
Yapo mambo mengi ambayo yameweza kuzungumzwa ambayo yanaweza kukusababishia wewe kusonga mbele kimaisha lakini hata ukisoma mambo mengi yanayohusu mambo ya kimaisha bila kuthubutu kufanya kitu unachotaka kufanya ni kazi bure.
Inabidi kuwatathimini watu ambao wanakuzunguka, kuanzia marafiki,
majirani, na hata baadhi ya ndugu.Kuna wengine hata ukimwangalia
sura yake tu anaonekana wazi kuwa hana furaha unapomwambia kuwa mambo
yako yanakwenda vizuri kwa sababu watu wengi wanapenda kusikia kuwa
unaishi maisha ya shida ndio wengi walivyo na wakijua hivyo ndio
unaongeza uoga wa kuthubutu kufanya kazi. Sijui kwa nini hii inatokea,
lakini achana na hao wewe kazana kubuni miradi mingi ili uwe na
maendeleo bora maana wao kukasirika haikuzuii kufanya mambo yako.
Mafanikio yako yanatokana na akili yako ulionayo maana wengine
wamekuwa wakisema kuwa ugumu wa maisha ndio kipimo chako cha akili yako.
Katika jamii tunakoishi utakua ushasikia watu wanalalamika kuwa maisha
ni magumu,na hawajui wafanyaje lakini nikwambie kuwa kipimo cha maisha
unacho hapo wewe mwenyewe na akili yako. Kama unajua kusoma na kuandika
ni tosha kabisa kwa wewe kujiendeleza.
Kwaiyo jamani ni vizuri ukakaa na kutathimini unatamani maisha yako
yaweje au unataka kuishi vipi au maisha yako yakae katika level gani ya
kimaisha hapa duniani? Kipimo cha maisha ambayo unataka kuishi unacho
wewe mwenyewe pia uoga wako ndo umaskini wako yawezekana hapo ulipo kaa
una wasiwasi ,una uoga ,unawaza una tathimini wakati nguvu unazo, sababu
unazo, elimu unayo vifaa pia unavyo. Ila… kwa kumalizia Kitu kimoja tu
unahitaji ndugu yangu. “JITUME”.
Ukitaka kuelewa hii angalia wiki nzima iliyopita kama umefanya kitu
ambacho kinaendana na mambo ambayo unataka kufaninikiwa maishani mwako.
Kama kipo Good… kama hakipo, basi anza kujituma leo… yaani leo
namaanisha anza kupanga mikakati, kama serikali inavyoweka mipango na
mikakati ya miradi yake kwa wananchi na wewe kaa chini tengeneza
mikakati ya maisha yako.
Kumbuka Unapanga mikakati ya maisha YAKO! Sio
ya jirani yako ambae anakusema sema kila siku au mlie kosana nae juzi.
PITIA NA HIZI PIA
>>> Tuzungumze yanayo tusibu na Kupata suluhisho.>>> Viashiria 6 ni kwa nini unatakiwa kubadili Maisha yako Leo.
>>> Furaha ya kweli inaletwa na wewe mwenyewe.
No comments:
Post a Comment