
Kamanda Polisi mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas amesema baada ya tukio hilo jeshi la polisi lilifanya uchunguzi na kuwakamata watu hao lakini mtunza bustani Ismail Swalehe amekiri kufanya mauajki hayo kwa tamaa ya fedha kiasi cha shilingi milioni tano na kati ya hizo milioni nne zimepatikana zikiwa zimefukiwa chini nje ya nyumba ya marehemu na kudai alimkata shingo kwa panga akiwa sebuleni anakunywa uji ili aweze kuelekea kazini.
Kamanda Sabas amesema uchunguzi wa jeshi la polisi pia umegundua panga moja liliokuwa na damu ambalo lilikutwa kwenye stoo ya nyumba ya marehemu vitu vingine ni taulo nne kitambaa cha mezani suruali ya mtuhumiwa ambazo zilifichwa kwenye migomba karibu na banda la kuku nyumbani kwa marehemu ambazo zinadaiwa ndiyo zilizo tumika kupigia deki baada ya kuuwawa.
No comments:
Post a Comment