Mshambuliaji Cristiano Ronaldo wa miamba ya soka ya nchini Hispania
Real Madrid ametumia fursa ya mapumziko ya sikukuu za krismasi
kutembelea nchini Marekani ambapo alitokea katika mechi ya mpira wa
kikapu nchini humo NBA Kati ya Miami Heat na Detroit Pistons.
Cristiano Ronaldo ambaye ndiye mwanasoka tajiri zaidi hivi sasa
alipokelewa kwa mapokezi mazuri huku akikabidhiwa jezi ya Miami Heat
iliyokuwa imechapishwa jina lake mgongoni, sanjari na namba 7 kuonesha
heshima kubwa aliyonayo staa huyo raia wa Ureno.
Ronaldo alikabidhiwa jezi hiyo pamoja na kushiriki utani na stori
pamoja na mchezaji wa kikapu wa NBA mwingereza Luol Deng ambaye alifunga
points 9 katika dakika 33 alizocheza Jumanne hii na baadae kushiriki
stori na Cristiano.
Katika mechi hiyo Miami walipoteza kwa taabu kwa points 93 kwa 92
katika mchezo uliokua mkali na wakuvutia, huku mashabiki wakifurahia
uwepo wa staa huyo wa soka na mshindi wa Ballon d’Or mara 3.
Baadaye Cristiano Ronaldo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika
kumshukuru Luol Deng mwingereza ambaye pia ni shabiki wa kutupwa wa
Arsenal, pamoja na kuishukuru klabu ya Miami kwa ukarimu wao.
Cristiano bado yuko nchini Marekani akijipumzisha kwa ajili ya
Christmas kwani bado Ana muda wa kutosha kabla ya kurudi Hispania kwa
ajili ya muendelezo wa ligi kuu nchini humo pamoja na michuano mingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment