09 December, 2015

Quick Rocka athibitisha kuwa na uhusiano na Kajala

post-feature-imageMsanii wa Bongo fleva, Quick Rocka na muigizaji wa Bongo movie, Kajala Masanja hawakuwahi kuthibitisha wenyewe hadharani kuwa wana uhusiano wa kimapenzi licha ya kuwepo na tetesi kuwa ni wapenzi.Quick amejikuta akilazimika kukiri hadharani juu ya uhusiano wao alipokuwa akikanusha taarifa kuwa wameachana. 
Akizungumzia sababu za kuamua kutoyaweka wazi maisha ya uhusiano wao, Quick amesema;
“Sometimes some things have to stay private maana mahusiano yanapokuwa public sana ndio maneno yanakuwa mengi so sometimes vitu ni better kuwa private kidogo ili kuwe na usisi ndani yake yeah we doing good…Maneno ya mtaani ni mengi ukweli wa ndani tunaujua wenyewe.” Alisema Quick Rocka kupitia Amplifaya ya Clouds Fm.

Kiungo wa Manchester United, Schweinsteiger yupo hatarini kufungiwa Mechi 3 za ligi kuu ya England

post-feature-imageKiungo wa Manchester United Bastian Schweinsteiger yupo hatarini kufungiwa Mechi 3 za ligi kuu ya England baada ya kufunguliwa Mashitaka na Chama cha Soka cha England FA , kwa kosa la Kinidhamu.

Schweinsteiger, mwenye Miaka 31, anadaiwa kumpiga Beki wa West Ham Winston Reid kwa Mkono wa Kushoto walipokuwa wakigombea Mpira wa Frikiki katika Dakika ya 40 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyomalizika 0-0 Jumamosi iliyopita.

Schweinsteiger amepewa hadi Alhamisi Saa 9 Mchana kukana au kukubali Mashitaka.
Refa wa Mechi hiyo, Mark Clattenburg, hakulitaja tukio hilo lakini aliongea na Wachezaji wote Wawili baada ya tukio lenyewe.

Katika Taarifa yao, FA imesema kuwa tukio hilo lilipitiwa na Marefa Watatu tofauti ambao kila mmoja aliafiki lilistahili Kadi Nyekundu na ndio maana wakafungua Mashitaka dhidi ya Schweinsteiger.

Laiti kama Refa Mark Clattenburg angelilitaja tukio hilo kwenye ripoti yake ya Mechi basi FA isingekuwa tena na mamlaka ya kulipitia na kumshitaki. Ikiwa Schweinsteiger atafungiwa Mechi 3 atazikosa Mechi za Ligi dhidi ya Bournemouth, Norwich City na Stoke City na kurejea kwenye Mechi na Chelsea.

Hata kama anakupenda sana hawezi kukwambia ukweli kuhusu haya mambo

post-feature-imageZile habari za nakupenda, nakupenda pia kila mtu anajua siku hizi na  ni kawaida kwa miaka ya sasa, kuitana baby, hubby,sweet,mpenzi, mahabuba na majina mengine mengi sio lazima niyataje yote, ila unajua huyo mahabuba wako hata kama anakupenda vipi kuna vitu hawezi kukwambia ukweli, kuna vitu katika mahusiano watu huwa wanafichana na hata kama mnaambiana basi mnadanganyana.

Mahusiano yako ya nyuma
Ni vigumu sana wapenzi kuelezana historia zao za mapenzi hasa inapokuja swala la umetembea na wangapi?  Hapa kama uliambiwa umedanganywa tafiti zinaonyesha wanaume ndo wanajua kudanganya kwenye swala hili kuliko wanawake japokuwa kwa asilimia kubwa wapenzi huwa hawaambiani ukweli kuhusu watu wangapi wameshakuwa na mahusiano nao ya kimapenzi. Kwahiyo ni bora usiulize usijisumbue.

Kipato   
Hapa inakuwa shida kidogo kwani hela haina mapenzi, haina undugu na ni mara chache ukute wapenzi wanajua mishahara au kipato cha mwenza wake, wapenzi wengi huwa wanafichana na wengine hata wanadanganya kuhusu madeni waliyonayo ni kawaida sana kwa mapenzi ya sasa hasa hali ya kipato ilivyo ngumu.

Kufurahia Tendo
Wapenzi wengi hawaambiani kweli hasa wanapo kutana kimwili, kama walifurahia au walichukia, wanawake wanasifika kwa kudanganya wameridhika, ila pia wanaume huwa hawasemi kama msichana hayuko vizuri kwenye game, na ndo maana watu baada ya kuachana ndo utasikia wanachafuana oooh wewe ulikuwa kama gogo na mara ooh wewe ulikuwa kama toothpick  mambo kama hayo.

Muonekano
Kuna wakati mtu anapoteza mvuto wake wa asili lakini inakuwa vigumu kwa wapenzi kuambiana ukweli labda mtu amenenepa sana, au amekuwa na kitambi sana na hana mvuto lakini sababu ya mapenzi au uoga inakuwa vigumu wapenzi hawa kuambiana ukweli

Matumizi ya Kilevi
Kwenye matumizi ya pombe baadhi huwa wanakuwa wawazi, lakini wapo wanaoficha matumizi mengine ya kilevi kama kuvuta sigara na matumizi ya miraa au mirungi,

Hisia zake kwa mpenzi wa zamani (EX)
Wapo watu wanaingia kwenye mahusiano wakiwa bado wana hisia za mapenzi  na wapenzi wao wa zamani lakini sio rahisi kusema hayo kwa wapenzi wao,na hata wakiulizwa huwa wanadanganya. Na sio  raisi kuleta habari za mapenzi ya nyuma kwa mpenzi mpya. Ni vigumu kukwambia  anavyojisikia jua ya mpenzi wake wa zamani.

Wanamuziki Justin Bieber na Taylor Swift watikisa twitter

post-feature-imageWanamuziki Justin Bieber na Taylor Swift ndio waliotamba zaidi kwa mazungumzo katika mtandao wa kijamii wa Twitter mwaka 2015, wakuu wa Twitter wamesema.Kwa miezi sita ya kwanza, Taylor Swift ndiye aliyetawala kabla ya Justin Bieber “kuchukua usukani”.

Lakini mazungumzo katika mtandao wa Twitter haujakuwa kuhusu wasanii pekee na muziki.
"Mazungumzo ya kisiasa na watu wakieleza hisia zao pia vimeongezeka,” mkuu wa Twitter Ulaya Bruce Daisley aliambia kipindi cha Newsbeat.

"Ndiye msanii wa tatu kwa kuwa na wafuasi wengi Twitter. Nusu ya pili ya mwaka, Justin Bieber alitawala,” anasema Daisley.

"Bieber ndiye wa pili kwa kuwa na wafuasi wengi. Alikuwa na wafuasi 50 milioni na amewatumia vyema na kwa werevu.”Ujumbe uliosambazwa mara nyingi zaidi kwenye Twitter ulikuwa wa kiongozi wa bendi ya One Direction Harry Styles.

Rais Magufuli na waziri mkuu Majaliwa waongoza Watanzania kufanya usafi

post-feature-image

Mamia ya watu walirauka na kuanza kusafisha baadhi ya maeneo ambayo hujulikana sana kwa kuwa na uchafu na taka kwa wingi. Mwandishi wa BBC Sammy Awami aliwapata wachuuzi na maafisa wa baraza la jiji Dar es Salaam asubuhi na mapema wakifanya usafi katika soko maarufu la Kariakoo.
Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pia amefika soko hilo la Kariakoo. Rais John Magufuli naye amekuwa kwenye aneo la ufuo wa bahari karibu na ikulu akiwa amevalia glavu. Katika eneo la Mwenge, wananchi pia wanajizatiti kufanya usafi. Mwandishi wa BBC Regina Mziwanda amewapata wananchi hawa wakiteketeza takataka baada ya kuzikusanya pamoja.

KLAY THOMPSON AWAKUMBUSHA WATU UWEPO WAKE, GOLDEN STATE WARRIORS MOTO CHINI, WASHIKA KALAMU YA NBA.

warr
Ni kama Golden State Warriors wameishikilia kalamu ya NBA. Ni kama Stephen Curry ameiba kamera za waandishi, lakini Klay Thompson alijaribu kuwakumbusha pia sio vyema kumsahau kirahisi vile. Warriors yaendelea kuonyesha sio timu ya kawaida na haibahatishi.
Vyombo vya habari huingia uwanjani vikitizama Curry yupo wapi lakini yeye huingia akitizama naipeleka wapi Golden State Warriors. Ndio maana mchezaji mwenzake akiwa moto haoni shida kumpa show aiendeshe. Ndicho alichofanya kwa Klay Thompson ambaye alimaliza mchezo akifunga pointi 39, rebound 7 na pasi 6 na Warriors wakashinda 131-123 dhidi ya Indiana Pacers.
Kila ukitizama namna Warriors wanavyocheza ni rahisi kuamini kuwa kuvunja rekodi ya Chicago ya kushinda michezo 72 kwa msimu ni jambo linalowezekana kabisa. Klay Thompson alifunga mitupo ya pointi 3 kumi kati ya 16 aliyojaribu. Stephen Curry aliongeza pointi 29, pasi 10 na rebound 7.
Paul George ameendelea kuwa na msimu bora ambapo aliiongoza Pacers kwa kufnga pointi 33, huku C.J Miles akifunga pointi 24.
war
REKODI ZILIZOWEKWA.
Stephen Curry sasa amefunga pointi 3 katika michezo 87 mfululizo, akifikia rekodi ya Rashard Lewis ya msimu wa 2007 mpaka 2009.
Warriors wameendelea kuimarisha rekodi yao bora ya kuanza msimu kwa michezo mingi mfululizo wakifikisha 23 sasa. Warriors pia wameshinda michezo 27 mfululizo ikiwemo 4 ya kumalizia msimu uliopita na sasa wamelingana na MiamiHeat ya msimu wa 2012-13 katika nafasi ya pili. Wamebakisha rekodi ya michezo 33 ya Los Angeles iliyowekwa msimu wa 1971-72.
Golden State Warriors sasa wameshinda michezo 13 mfululizo ya ugenini, ya kufungua msimu.  Wamevunja rekodi ya michezo 12 mfululizo waliyokuwa wamelingana na New York Knicks.
Warriors wamevuka pointi 100 katika michezo yote 23 waliyocheza msimu huu, wamefanya hivyo kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1966-67.
Warriors imekuwa ni timu ya kwanza katika timu zote zinazoshiriki michezo katika mashindano ya michezo yote marekani ikiwemo Hockey, Baseball, American Football na NBA kuwahi kushinda michezo 16 mfululizo katika misimu miwili mfululizo.

08 December, 2015

Utafiti uliofanywa umeonyesha Unene wa mwanaume huathiri mbegu za kiume

post-feature-image
Utafiti uliofanywa nchini Denmark umeonyesha uzani wa mwanamume huathiri seli za mbegu za kiume na huenda ukachangia katika kuwafanya watoto wanaozaliwa kuwa wanene

Seli za mbegu za kiume za wanaume wembamba na wanaume wanene zilikuwa na taarifa tofauti za kijenetiki, jambo ambalo huenda linaathiri utendaji wa chembe za kijenetiki.

Dkt Romain Barres, aliyesaidia katika utafiti huo alisema awali ilikuwa imebainika kwamba: “Mwanamke anapokuwa mjamzito anafaa kujitunza vyema. Lakini utafiti huu unaonyesha wanaume wanafaa pia kuangalia uzani wao.”

Utafiti huo ulifanywa kwa wanaume sita walionenepa kupindukia na ambao walikua wakisaidiwa kupunguza uzani. Watafiti walichunguza mbegu za kiume za wanaume hao kabla na baada ya kupunguza uzani baada ya mwaka mmoja.

Dkt Romain Barres mtafiti mkuu wa ripoti hii amesema waligundua tofauti iliyokuwepo kwa wanaume hao. Utafiti unasema kwamba zeli za mbegu za wanaume walionenepa husababisha mabadiliko ya tabia.

Aidha ripoti imeonya wanawake walio na mimba kuwa waangalifu sana hasa ikiwa walitunga mimba hizo wakiwa na wanaume walionenepa sana. Dkt Barres amesema wanaume walionenepa sana husababisha jeni zao kuanza kutamani kula chakula kila mara.

Ameongeza kwamba uzani wa mtu pia unaambatana na ukuaji wa akili. Utafiti huu uliochukua miaka mitano pia ulitofautisha wanaume 13 wenye uzani wa kadiri na 10 walionenepa zaidi. Hapo ikagunduliwa kwamba, wote walikua na tabia tofauti na zilizochochewa na mabadiliko ya seli kwenye mbegu za kiume.

Utafiti pia unasema uzani wa baba unaweza kusaidia, wanawe. Utafiti unasema kwa kula sana baba watoto pia huwahimiza wanawe kula sana ili wakue kwa haraka. Prof Allan Pacey amesema utafiti huu umebainisha kwamba baadhi ya tabia za watoto zimechangiwa na zilizokua mbegu za kiume za baba yao


Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...