Kiungo wa Manchester United Bastian Schweinsteiger yupo hatarini
kufungiwa Mechi 3 za ligi kuu ya England baada ya kufunguliwa Mashitaka
na Chama cha Soka cha England FA , kwa kosa la Kinidhamu.
Schweinsteiger, mwenye Miaka 31, anadaiwa kumpiga Beki wa West Ham
Winston Reid kwa Mkono wa Kushoto walipokuwa wakigombea Mpira wa Frikiki
katika Dakika ya 40 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyomalizika 0-0
Jumamosi iliyopita.
Schweinsteiger amepewa hadi Alhamisi Saa 9 Mchana kukana au kukubali Mashitaka.
Refa wa Mechi hiyo, Mark Clattenburg, hakulitaja tukio hilo lakini aliongea na Wachezaji wote Wawili baada ya tukio lenyewe.
Katika Taarifa yao, FA imesema kuwa tukio hilo lilipitiwa na Marefa
Watatu tofauti ambao kila mmoja aliafiki lilistahili Kadi Nyekundu na
ndio maana wakafungua Mashitaka dhidi ya Schweinsteiger.
Laiti kama Refa Mark Clattenburg angelilitaja tukio hilo kwenye ripoti
yake ya Mechi basi FA isingekuwa tena na mamlaka ya kulipitia na
kumshitaki. Ikiwa Schweinsteiger atafungiwa Mechi 3 atazikosa Mechi za
Ligi dhidi ya Bournemouth, Norwich City na Stoke City na kurejea kwenye
Mechi na Chelsea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment