Wanamuziki Justin Bieber na Taylor Swift ndio waliotamba zaidi kwa
mazungumzo katika mtandao wa kijamii wa Twitter mwaka 2015, wakuu wa
Twitter wamesema.Kwa miezi sita ya kwanza, Taylor Swift ndiye
aliyetawala kabla ya Justin Bieber “kuchukua usukani”.Lakini mazungumzo katika mtandao wa Twitter haujakuwa kuhusu wasanii pekee na muziki.
"Mazungumzo ya kisiasa na watu wakieleza hisia zao pia vimeongezeka,” mkuu wa Twitter Ulaya Bruce Daisley aliambia kipindi cha Newsbeat.
"Ndiye msanii wa tatu kwa kuwa na wafuasi wengi Twitter. Nusu ya pili ya mwaka, Justin Bieber alitawala,” anasema Daisley.
"Bieber ndiye wa pili kwa kuwa na wafuasi wengi. Alikuwa na wafuasi 50 milioni na amewatumia vyema na kwa werevu.”Ujumbe uliosambazwa mara nyingi zaidi kwenye Twitter ulikuwa wa kiongozi wa bendi ya One Direction Harry Styles.
No comments:
Post a Comment