09 December, 2015

Rais Magufuli na waziri mkuu Majaliwa waongoza Watanzania kufanya usafi

post-feature-image

Mamia ya watu walirauka na kuanza kusafisha baadhi ya maeneo ambayo hujulikana sana kwa kuwa na uchafu na taka kwa wingi. Mwandishi wa BBC Sammy Awami aliwapata wachuuzi na maafisa wa baraza la jiji Dar es Salaam asubuhi na mapema wakifanya usafi katika soko maarufu la Kariakoo.
Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pia amefika soko hilo la Kariakoo. Rais John Magufuli naye amekuwa kwenye aneo la ufuo wa bahari karibu na ikulu akiwa amevalia glavu. Katika eneo la Mwenge, wananchi pia wanajizatiti kufanya usafi. Mwandishi wa BBC Regina Mziwanda amewapata wananchi hawa wakiteketeza takataka baada ya kuzikusanya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...